Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, April 8, 2015

UKURASA WA 98; Usibabaishwe Na Watu.

Katika kitu kimoja unachoweza kufanya kwenye maisha yako leo na ukapata ahueni kubwa sana ni kuacha kuangalia wengine wana nini au wanafanya nini.

Kuna wakati ambapo unaona kama watu wengine wanamaisha mazuri kuliko uliyonayo wewe. Unaweza kuona watu wanamagari mazuri kuliko ulilonalo wewe au huna kabisa. Unaweza kuona wengine wana majumba mazuri kuliko uliyonayo wewe.

Hii inaweza kukufanya ujione kama wewe kwenye haya maisha unacheza au hujui ni nini hasa unachofanya. Hapa ndio unafanya makosa makubwa sana kwenye maisha yako.

SOMA; Hiki Ndio Kitu Kitakachokuletea Mafanikio Ambacho Tayari Unacho.

Kwanza kabisa sio kila unachoona kiko kama kinavyoonekana.

Pili sio kila kitu ambacho watu wanakuambia ni kweli.

Tatu kila mtu anapend akuonekana ana maisha bora kuliko ya wengine.

Sasa wewe ondoka kwenye kundi hili kubwa la watu wanaoishi maisha ya kuigiza. Anza kuishi maisha yale ambayo umeyapangilia. Nunua vitu ambavyo unahitaji kweli kuvitumia. Na chagua maisha ambayo umeridhika nayo. Kamwe usijilinganishe na watu wengine. Hakuna anayeweza kukupangia maisha bora ni yapi, wewe ndio unayepanga.

SOMA; Huu Ndio Mtaji Mkubwa Ambao Tayari Unao.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba maisha bora ni yale ninayochagua mimi kuishi. Najua kwamba kile ninachoona au kusikia kwa wengine sio uhalisia, wakati mwingine watu wanadanganya kwa sababu wanataka kuonekana wana maisha bora. Sitababaishwa na haya yote. Nitaweka nguvu zangu kwenye malengo na mipango yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 99 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment