Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, April 28, 2015

UKURASA WA 118; Kitu Pekee Kinachoweza Kuiharibu Siku Yako Na Jinsi Unavyoweza Kuepuka…

Kuna watu huwa wanasema kwamba siku zao zina kisirani, wengine husema wameamkia upande mbaya na maneno mengine mengi yanayoashiria kwamba kuna siku mbaya na siku nzuri.

Tuchukue mfano, umeamka asubuhi na kwa bahati mbaya umeamka kwa kuchelewa, hivyo unaanza kujiandaa haraka haraka, unavaa nguo huku unafanya mambo mengine ili tu uokoe muda. Mara asubuhi hiyo ukapishana kauli na mtu wa karibu unayeishi nae, anaweza kuwa mke/mume, mtoto au hata rafiki. Unapata hasira sana na hata kumwambia maneno makali. Unatoka na kufika barabarani, labda unatumia daladala kama usafiri na unakuta daladala hakuna, zinakuja zimejaa na unatakiwa kugombania.

SOMA; USHAURI; Jinsi Unavyoweza Kuondokana Na Changamoto Za Kuendesha Biashara Na Kuweza Kufikia Mafanikio Makubwa

Unagombania na kupata daladala, mara kidogo katika kukaa vizuri mtu anakukanyaga, unamuuliza kistaarabu kwa nini anakanyaga tu bila kuangalia? Anakujibu ungekuwa unataka raha ungepanda teksi au ungenunua gari lako. Maneno hayo yanakuw amachungu sana kwako, mnajibizana tena maneno makali. Wakati huo huo kuna foleni ndefu sana halafu unaona trafic anaita magari mengine kwa muda mrefu ila ya upande mliopo hayaitwi kabisa. Unazidi kupata hasira.

Unafika ofisini, hapo tayari umechelewa. Unakuta bosi wako anakusubiri kwa hamu na kuanza kukusem akw atabia yako ya kuchelewa. Unajaribu kujitetea ndio unawasha moto kabisa.

Sasa hebu niambie kwa siku kama hii unaweza kufanya kazi yoyote ya maana? Kwa hasira zote hizi ulizokusanya kuanzia nyumbani zinakutosha kutangaza kwamba hii ni siku ya kisirani. Na kila kazi utakayojaribu kufanya utakosea au kuibua mabishano na wengine.

Hebu kwanza tuanze na siku ya kisirani, je kuna siku maalumu ambayo ni ya kisirani? Na siku hiyo jua huwa linachomozea upande upi? Na urefu wa siku hiyo unakuwa masaa mangapi?

SOMA; Siri Hii Itakusaidia Kuondokana Na Msongo Wa Mawazo Wa Kukosa Muda Katika Ulimwengu Huu Wa Utandawazi - 2

Kwa kweli hakuna siku maalumu ambayo ni ya kisirani, siku zote zipo sawa, ila sisi wenyewe ndio tunaamua kufanya baadhi ya siku zetu kuwa za kisirani. Kitu pekee kinachoweza kuharibu siku yako na kuifanya kuwa ya kisirani ni watu. Ila wewe ndiye utakayetoa ruhusa ya watu kuharibu siku yako. Kwa mfano unapoamka umechelewa, tayari umechelewa, hivyo hata kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja hakukufanyi uwahi. Kama mtu amekujibu vibaya, huna haja na wewe kumjibu vibaya, huenda na yeye amechelewa kama wewe au ana hasira zake nyingine, sasa wewe unapokubali kuingia kwenye majibishano nae unakuwa umemruhusu aharibu siku yako pia.

Kitu pekee kinachoweza kuharibu siku yako ni watu. Na njia bora ya kuepuka hili ni kutokuruhusu watu walete matatizo yao kwenye siku yako. Kama mtu anafanya jambo lolote la kukuudhi, achana naye, mpuuzie na wewe kazana kuifanya siku yako iwe bora, kwa kufanya kazi yako kwa ubora wa hali ya juu. Kumbuka mafanikio yako hayatokei siku moja, bali ni muunganiko wa siku nyingi ambazo umeishi kwa mafanikio. Linda sana siku yako, usirihusu watu waiharibu.

SOMA; Hivi Ndivyo Unavyokaribisha Ushindani Kwenye Biashara Yako.

TAMKO LA LEO;

Najua watu wanaweza kuiharibu siku yangu kama nitawapa ruhusa hiyo. Kuanzia sasa sitatoa tena ruhusa kwa mtu kuiharibu siku yangu. Nitailinda siku yangu kwa sababu najua kila siku inachangia kwenye mafanikio yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 119kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment