Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, April 9, 2015

UKURASA WA 99; Fanya Kama Hakuna Anayekuangalia.

Kila mmoja wetu anapenda kufanya jambo fulani ambalo huenda watu wengine hawafanyi. Lakini kikwazo kikubwa kinachowazuia watu kufanya jambo hilo ni kuona wataonekanaje na watu wengine.

Watu wanaogopa kukosolewa, kupingwa na hata kukatishwa tamaa. Hofu hii imewazuia watu wengi kuishi maisha ya ndoto zao na kujikuta wakiishi kama ambavyo kila mtu kwenye jamii anaishi.

SOMA; Hakuna Anayejali Maisha Yako Zaidi Yako Mwenyewe.

Mtoto mdogo, chini ya miaka saba, huwa haogopi kufanya chochote, huwa haogopi kusema chochote. Hii ni kwa sababu bado hawajaijua hukumu inayoendelea kwenye jamii zetu. Wako huru kufikiria na kufanya chochote wanachopenda. Lakini tunapokua tunaanza kuhukumiwa, usifanye hiko, wenzako walijaribu wakashindwa, huwezi, kuwa tu na maisha ya kawaida na mengine mengi.

Kuna mtu hawezi kucheza mziki mbele ya watu ila akiwa mwenyewe anaweza kucheza mziki kama anavyotaka mwenyewe. Hii ni kwa sababu anajua hakuna wa kumhukumu, anajua yupo huru kufanya kile anachotaka kufanya, bila ya kukatazwa au kukatishwa tamaa.

SOMA; Unajaribu Kumdanganya Nani?

Hiki ndio unachotakiwa kufanya kwenye maisha yako, fanya kitu kama vile hakuna mtu anayekuangalia. Fanya kwa moyo wako wote na weka akili zako zote. Hata kama kuna wanaokuangalia na kukukatisha tamaa wewe usiwasikilize, endelea kufanya kama hakuna anayekuona. Najua ni vigumu lakini kama umedhamiria kweli hakuna kitakachoshindikana.

TAMKO LA LEO;

Nimeshachagua ni kitu gani nitafanya kwenye maisha yangu. Najua kuna wengi wananikatisha tamaa na kunirudisha nyuma. Nimeamua kufanya kile ninachofanya kama vile hakuna mtu yeyote anayeniangalia. Kwa njia hii nitakuwa huru kufanya kile ambacho ninataka kufanya.

SOMA; Ingia Kwenye Biashara Yenye Ushindani Lakini Usishindane.

Tukutane kwenye ukurasa wa 100 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment