Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, April 7, 2015

UKURASA WA 97; Hakuna Kitu Kizuri Au Kibaya.

Mambo mengi yanayotokea kwenye maisha yako hayana maana kabisa. Japo wewe unaweza kuona kitu fulani ni kibaya au kitu kingine ni kizuri, ukweli ni kwmaba hakuna kitu kama hiko.

Kila kitu kipo kama kilivyo, uzuri au ubaya wa kitu unatokana na mtizamo wako mwenyewe. Kinapotokea kitu, mtizamo wako na mawazo yako ndio vitahukumu kama kitu hiki ni kizuri au ni kibaya.

SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.

Kwa mfano ikatokea ndugu yako amepata kesi mahakamani na kesi hii ameshtakiwa na mtu mwenye fedha nyingi(tajiri). Ikatokea tajiri yule ameshind akesi na ndugu yako amefungwa au kukosa haki basi utasema mahakama ni mbaya sana kwa sababu inawapa haki wenye fedha. Ikitokea siku nyingine wewe una kesi na mtu ambaye naye ana fedha nyingi au ana nguvu na ukashinda kesi ile, utasema mahakama inatenda kazi kwa haki na usawa.

SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.

Hivi ndivyo ilivyo kwenye kila eneo la maisha yetu. Pale linapotokea jambo linaloendana na mawazo yetu tunasema ni zuri na pale linapotokea jambo lisiloendana na mawazo yetu tunasema ni baya.

Hata kwenye uchaguzi, chama tunachoshabikia kikishinda tunasema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki. Ikitokea chama kingine kimeshinda tunasema uchaguzi umechakachuliwa. Hata timu za mpira, timu yako ikipata penati unasema penati ilikuwa ya haki, timu pinzani ikipata penati tunasema wamepewa penati.

Hata shuleni, mwanafuzni akipata A anasema nimepata A, nimefaulu. Akipata Cau D anasema mwalimu kanipa C au D.

Usitake kubadili jambo, badili mtazamo wako juu ya jambo lolote na maisha yako yatabadilika.

SOMA; BIASHARA LEO; Tumia Kigezo Hiki Katika Bei Ili Uweze Kufanikiwa.

TAMKO LA LEO;

Najua ya kwamba hakuna kitu chochote chenye maana bali mimi mwenyewe ndio naweka maana kwenye vitu. Najua maana yoyote nayoweka kwenye kitu au jambo inatokana na mtazamo nilionao na mawazo yangu. Nitabadili mtazamo wangu ili niweze kuona kile ninachotakiwa kuona.

Tukutane kwenye ukurasa wa 98 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment