Kuna wakati kwenye maisha huwa tunatamani watu wawe kama vile ambavyo sisi tunataka. Tunataka watu wawe na tabia zile tunazotaka na tunataka wafanye kile ambacho tunataka wafanye.
Kwa kufanikisha hili, tunajaribu kuwabadili, tunawawekea masharti fulani ili wabadilike. Lakini je tunaambulia nini? Hatuambulii chochote.
SOMA; Ukweli Kuhusu Maisha Ambao Kila Mtu Anapaswa Kuujua.
Kama kuna kitu ambacho watu hawapendi ni kulazimishwa kubadilika. Kila mtu anataka aone maisha yake ni muhimu kwake na hakuna anayempangia nini cha kufanya. Wewe unapojaribu kumbadili, tena kwa nguvu unamfanya awe mkali sana na ahakikishe uhuru wake anautetea.
Una mke/mume ambaye ana tabia ambazo huzipendi, unakazana kuzibadili. Lakini unaishia kushindwa kufanya hivyo. Una rafiki ambaye ungetamani awe tofauti na alivyo sasa, lakini ukijaribu kumbadili huwezi. Yote hii ni kwa sababu hiyo hapo juu.
Sasa unafanya nini?
1. Wakubali watu walivyo, usilazimishe mtu kubadilika.
2. Kama unaona kuna mabadiliko yanahitajika, mshauri mtu, muoneshe ni jinsi gani ambavyo akifanya kitu kw autofauti itakuwa faida kwake na kwako pia.
3. Usiweke mategemea makubwa kwa watu. Wape watu nafasi ya kukosea. Usiweke masharti kwa watu, kwamba ukifanya hivi ndio nitakupenda, kama unamkubali mtu mkubali alivyo.
4. Badilika wewe kwanza, na utaona mabadiliko makubwa kwa wengine. Hata kama hutabadilika tabia, badili mtazamo wako juu ya wale unaotaka wabadilike.
TAMKO LA LEO;
Najua ni vigumu sana kubadili watu. Sitapoteza muda wangu kutaka kuwabadili watu, nitawashauri wabadilike kwa sababu itakuwa na faida kwao na kwangu pia. Na hata kama hawatabadilika, sitakuwa na tatizo nao.
Tukutane kwenye ukurasa wa 107 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment