Kitu chochote unachotaka kwenye maisha yako, unaweza kukipata na pia unaweza kukikosa. Kama hutaweka juhudi kwa hakika utakikosa. Kama ukiweka juhudi kupitiliza pia unaweza kukikosa.
Njia nzuri na ya uhakika ya kupata chochote unachotaka na maisha yako kuendelea kuwa bora ni kufanya kwa kiasi. Usifanye kwa chini sana na usifanye kwa juu sana. Fanya kwa kiasi na mambo yako yatakwenda vizuri.
SOMA; BIASHARA LEO; Kwa Nini Watu Hawawaambii Wengine Kuhusu Biashara Yako.
Ndio najua kwamba unataka kufikia uhuru wa kifedha, lakini kufanya kazi masaa 20 kwa siku sio njia nzuri ya kukufikisha kwenye uhuru huu.
Ndio najua unataka kupata starehe, lakini kunywa pombe mpaka unalewa kila siku hiyo sio starehe tena.
Ndio nakubali kwamba upo bize ili kufikia malengo yako, lakini kuwa bize mpaka unakosa muda wa muhimu kwako na wale wanaokuzunguka hakutayafanya maisha yako yawe bora.
Na ndio najua unataka kufanya mazoezi, lakini kukimbia kilomita 10 siku ya kwanza ya mazoezi kutakufanya kesho yake ushindwe kabisa kufanya mazoezi.
SOMA; Tabia Hizi Zitakusaidia Sana Kufikia Malengo Yako Kwa Haraka - 2
Kula kwa kiasi, fanya mapenzi kwa kiasi, amini kwa kiasi.
Chochote unachofanya kwenye maisha yako fanya kwa kiasi. Kupitiliza kiasi kunaweza kuharibu maisha yako zaidi.
Angalizo; usiweke kiasi kwenye kile unachozalisha, unatakiwa kukifanya kuwa bora kila siku. Kumbuka kama unafanya kazi ya kiasi yaani ya kawaida maana yake unafanya kazi ya hovyo. Weka kiasi kwenye maisha yako, lakini sio kwenye kile unachozalisha.
TAMKO LA LEO;
Chochote nitakachofanya kwenye maisha yangu nitafanya kwa kiasi. Najua nikipitiliza sana nitajiweka kwenye matatizo makubwa zaidi.
SOMA; Jinsi ya kuzuia hatari ya kupata hasara kupitia uwekezaji katika hisa
Tukutane kwenye ukurasa wa 96 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment