Kama unaweza, huna haja ya kupiga kelele ili uonekane kwamba unaweza. Njia rahisi ya wewe kuonesha wkamba unaweza ni kufanya kile ambacho unaweza, tena ukifanye kwa ubora wa hali ya juu sana kuliko ambavyo imewahi kufanya na mtu mwingine yeyote.
Kuwapigia watu kelele kwamba unaweza, kutaka na wewe uonekane kwamba unaweza ni kupoteza muda mzuri ambao ungeweza kuutumia kufanya kile ambacho kinaonekana kwa kila mtu.
SOMA; Huu Ndio Mtaji Mkubwa Ambao Tayari Unao.
Kuna usemi unasema kwamba matendo yanaongea kwa sauti kuliko maneno. Hivyo ni vyema sana kuonesha vitendo kuliko kupiga kelele.
Kuongea ni rahisi sana, hata kasuku anaweza kuongea. Kufanya ndio kinatuonesha kwamba ni nani anayeweza kweli na ni nani ambaye anapiga kelele tu. Kwenye jambo lolote unalofanya kunakuwa na changamoto nyingi, hivyo kama umeweza kukamilsiha jambo tunaamini wkamba umeweza kuvuka changamoto hizi na hivyo una kitu kikubwa ndani yako.
Usiseme kwamba unapenda kufanya biashara, unataka kufanya biashara, ingia kwenye biashara, anza hata kama ni kidogo kiasi gani, kua na watu watakuona. Badala ya kuwapigia watu kelele kwamba kama ungepata mtaji ungefanya baishara, hebu waoneshe ni kipi umeweza kufanya ili washawishike kukuongezea mtaji.
SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.
Kila mtu anaweza kusema kwamba akipata mtaji atafanya biashara, hata mtoto mdogo anaweza kusema hivyo. Sasa na wewe kusema hivi hakukupi tofauti yoyote na wala hakukuweki kwenye nafasi ya kupata mkopo huo. Onesha vitendo ambavyo vitawashawishi watu kwamba kama ukiongezea mtaji utakwenda mbali zaidi ya pale ambapo tayari umefika.
Usipige kelele kwamba kama ukiongezewa mshahara utafanya kazi kwa ubora au wka kiwango cha juu. Kila mtu anaweza kusema hivyo. Hebu anza kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu, anza kuweka thamani kubwa kwenye kazi yako na utashawishi kuongezewa mshahara.
Usipige kelele, fanya watu waone.
SOMA; BIASHARA LEO; Ingia Kwenye Biashara Yenye Ushindani Lakini Usishindane.
TAMKO LA LEO;
Najua kusema ni rahisi sana, sitaingia kwenye kundi hilo la wasemaji. Kama kuna kitu chochote ambacho nataka watu wajue kuhusu mimi, sitakazana kusema, bali nitakazana kufanya na najua wataona kile ninachofanya.
Tukutane kwenye ukurasa wa 101 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment