Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, April 30, 2015

UKURASA WA 120; Ni Muda Tu…

Nafikiri umewaona watu wengi ambao wamefanikiwa zaidi ya ulivyofanikiwa wewe. Na labda kuna wakati unajiona wewe umeshindwa kwa sababu tu hujafikia viwango vile ambavyo wengine wameweza kufikia. Au labda huna uwezo mkubwa, au labda huna bahati kama waliyonayo wengine.

Yote haya sio ya kweli, hakuna mwenye bahati zaidi ya mwenzake na mafanikio hayatrofautiani kwa uwezo. Kama unafanya kile ambacho unahitaji kufanya ili kuwez akufikia mafanikio unayotaka, basi kuna kipimo kimoja kikubwa kati ya waliofanikiwa na ambao bado hawajafanikiwa, nacho ni MUDA.

SOMA; Sema HAPANA, Hapa Ndio Uhuru Wako Ulipo.

Hata kama una mipango mizuri kiasi gani, hata kama unafanya akzi kwa juhudi na maarifa kiasi gani, hata kama una una nidhamu na uvumilivu mkubwa sana, bado mafanikio hayatakuja haraka kama mvua. Unahitaji muda wa kuyafanyia kazi ndio uweze kuyaona mafanikio hayo.

Watu wote ambao unawaona wamefanikiwa wamekuwa wakifanya kitu hiko kw amuda mrefu na hivyo wameshafanya makosa mengi na  kujifunza. Wameshajijengea uzoefu mkubwa na wanaweza kuutumia vizuri na kuwawezesha kufikia mafanikio.

SOMA; Hivi Ndio Vitu Vinavyopelekea Ongezeko La Thamani Ya Hisa Kwa Mwekezaji.

Usiumie kwa sababu umeanza kufanya kitu mwaka mmja au miwili iliyopita na bado huoni mabadiliko. Bado unahitaji kuweka muda zaidi. Usiingie kwenye biashara leo na kujilinganisha na aliyekuwepo kwenye biashara kw amiaka kumi sasa, tayari yeye ameshatengeneza mzingi imara zaidi.

Chochote unachofanya kwenye maisha yako, jua kwmaba unahitaji muda ili kuweza kufikia mafanikio. Mafanikio ni mkusanyiko wa mambo madogo madogo ambayo yamefanywa kwa muda mrefu. Endelea kufanya mambo madogo madogo kwa ufanisi mkubwa na mwisho wa siku utaona mabadiliko makubw akwenye maisha yako.

SOMA; Usipoteze Muda Kwa Vitu Vidogo Vidogo.

TAMKO LA LEO;

Najua muda ndio tofauti pekee kati ya waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa bado, kama wote wanafanya kile ambacho wanahitaji kufanya ili wafanikiwe. Nitaendelea kuweka juhudi na maarifa kwenye malengo na mipango yangu kwa sababu najua baada ya muda nitakuwa mbali sana na hapa nilipo sasa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 121 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

 

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment