Leo ni siku ya mwisho ya kujiunga na SEMINA YA MAFANIKIO KUPITIA BIASHARA. Kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA.
Kwa kiasi kikubwa sana umepoteza uhuru wako kwenye maisha. Kumbuka kipindi ulipokuwa mtoto ni mambo gani uliyokuwa unafikiria au kupanga? Ni ndoto zipi kubwa ulizokuwa nazo ambazo hukuona haya kuzisema mbele ya watu? Vipi kuhusu leo hii? Bado una ndoto zile? Unazifanyia kazi?
Kwa watu walio wengi sana jibu ni hapana. Na wengi watasema zile zilikuwa akili za kitoto tu, mambo niliyokuwa nasema hayawezekani. Unaweza kujiaminisha hivi ila ukweli ni kwmaba ulipokuwa mtoto ulikuw ana uhuru mkubwa wa kufikiri na kusema chochote, ila ulivyoendelea kukua ulianza kupoteza uhuru wako na badala yake ukalazimishwa kufikiri na kufanya kama ambavyo kila mtu kwenye jamii yako anafikiri.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutengeneza Biashara Kubwa Kwa Kuanzia Chini Kabisa, Hata Kama Huna Kitu.
Kama bado unasisitiza zile zilikuwa akili za kitoto, sawa nakubaliana na wewe kwa muda. Turudi kwenye malengo uliyojiwekea mwaka huu. Leo ni tarehe 01/05/2015 tunakaribia sana kufika nusu ya mwaka. Je kwa malengo uliyojiwekea mwaka huu umeshakaribia kufikia nusu? Je kwa miezi iliyopita umefanikiwa kufikia hatua ulizojiwekea? Kwa watu wengi jibu ni hapana. Sasa swali litakuja tena kwako, ni nini kinakuzuia wewe kufikia malengo ambayo umejiwekea wewe mwenyewe?
Kuna vitu viwili ambavyo vinakunyima wewe uhuru mkubwa wa kuweza kufanya kile unachotaka kufanya kwenye maisha yako. Vitu hivyo ni HOFU na KUTAFUTA SABABU.
Kwa mfano lengo lako ni kuanzisha na kukuza biashara yako kwa kiwango cha juu sana. Baada ya kuweka lengo kama hili unatakiw akufuata utekelezaji, au sio? Sasa unapofika wakati wa utekelezaji ni nini kinatokea?
Kwanza HOFU anabisha hodi, anakuja kukuambia kuna uwezekano mkubwa wa wewe kupata hasara, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kushindwa, watu watakushangaa, hakuna atakayekubali kufanya biashara na wewe na mengine mengi. Wakati hofu anaendelea kukupa sera zake, ndugu yake SABABU naye anabisha hodi. Sababu anaanza kukuambia, huwezi kufanya biashara KWA SABABU huna mtaji. Huwezi kufanikiw kwenye biashara hiyo KWA SABABU wengi waliofanya wameshindwa. Hutafikia malengo hayo KWA SABABU huna muda wa kutosha. Unawasikiliza watu hawa wawili na nini kinatokea? Unapoteza kabisa uhuru wako, unashindwa kupiga hatua yoyote na unabaki hapo ulipo.
SOMA; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Ili Uwe Tajiri.
Leo nataka nikushirikishe njia moja itakayokuwezesha kupata uhuru wako ulioupoteza siku nyingi. Leo nakupa mbinu ambayo itawafanya ndugu hawa wawili, HOFU na SABABU wakusahau kabisa na wewe uweze kuendelea na mambo yako bila ya kubugudhiwa. Na mbinu hii ni rahisi sana kufanya.
Vifaa unavyohitaji kw aajili ya tukio hili; KARATASI, KALAMU, KIBERITI. Hatua za kufuata; Chukua karatasi na kalamu na upande wa kwanza wa karatasi orodhesha HOFU zote ambazo zinakuzuia wewe kuchukua hatua au kufikia mafanikio makubwa. Upande wa pili wa karatasi andika SABABU zote zinazokufanya usichukue hatua, hakikisha hakuna kinachobaki kwneye kichwa chako ambacho hujakiandika. Baada ya kufanya hivi, soma HOFU na SABABU hizo kwa sauti kisha chukua kiberiti na ichome karatasi hiyo moto. Wakati karatasi hiyo inateketea ona zile hofu na sababu zikiteketea na kukuacha wewe huru.
Sasa anza kufanyia malengo na mipango yako kazi. Kama HOFU au SABABU itajitokeza tena, kumbuka kwamba umeshavichoma moto na havina nguvu tena ya kukuzuia wewe.
Fanya zoezi hili leo na uandike historia mpya kwenye maisha yako. Au usilifanye na uendelee kuwa mtumwa wa HOFU na SABABU. Chaguo ni lako.
SOMA; Kijana Punguza Mambo Haya Ili Uweze Kupata Mtaji Wa Kuanza Biashara - 2
TAMKO LA LEO;
Leo nimeondokana na hofu na sababu zote ambazo zimekuwa zinanizuia kufanya mambo makubwa kwenye maisha yangu. Sina tena kikwazo, nipo tayari kufanya jambo lolote ambalo nimepanga kufanya. Mafanikio ni yangu, hakuna cha kunizuia.
Tukutane kwenye ukurasa wa 122 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment