Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, May 28, 2015

UKURASA WA 148; Mambo Kumi(10) Unayotakiwa Kubadili Leo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.

Kuna picha moja ya katuni ambapo kiongozi amesimama jukwaani na anawauliza wananchi, wangapi wanataka mabadiliko? Wote wananyoosha mikoni. Anauliza swali la pili wangapi wanataka kubadilika? Hakuna hata mmoja ananyoosha mkono.
Hivi ndivyo maisha ya watu wengi yalivyo, kila mtu anataka mabadiliko, anataka maisha yake yawe bora, anataka kuwa na kazi au biashara nzuri, anataka kuwa na familia bora, anataka kuwa na uongozi mzuri na mengine mengi mazuri. Lakini inapokuja swala kwamba inabidi mtu abadilike hapo ndio changamoto inapoanza.
SOMA; MUDA–Kitu Chenye Thamani Kubwa Ila Kisichothaminika Na Wengi.
Hakuna ambaye anataka kubadilika, japo kila mtu anataka mabadiliko. Kila mtu anataka aendelee kufanya kile ambacho amezoea kufanya, anataka kuendele ana masiah ambayo ameyazoea, lakini anataka kuona mabadiliko makubwa. Hii ni ndoto ya mchana ambayo haiwezi kutokea kwa njia yoyote ile.
Mabadiliko yanaanza na wewe na ndio vitu vingine vinabadilika. Unabadilika kwanza wewe na ndio kazi yako, biashara yako, mwenza wako, watoto wako, wafanyakazi wako na jamii inayokuzunguka wanabadilika. Haiendi kinyume na hapo, kwamba hivyo vingine vyote vikishabadilika basi na wewe ndio utabadilika, usipoteze muda wako, hakuna kitu kama hiko.
Unataka kufikia mafanikio makubwa kwneye maisha yako? Haya hapa ni mabadiliko kumi unayotakiwa kuyafanya sasa, yaani leo hii hii kama bado umekuwa huyafanyi.
1. Kuwa na matumizi mazuri ya muda wako, usiupoteze kwa mambo yasiyokuw aya msingi kwako.
2. Usishiriki kwenye majungu, umbeya au kumsema mtu vibaya.
3. Weka juhudi kubwa sana kwenye kazi yako, nenda hatua ya ziada, fanya zaidi ya mtu mwingine yeyote.
4. Acha matumizi mabovu ya fedha, nunua vitu ambavyo ni muhimu kwako.
5. Acha kukaa na watu ambao wanakurudisha nyuma.
SOMA; Mitandao Ya Kijamii, Kazi na Mapumziko.
6. Pata muda wa kukaa na familia yako na wale unaowapenda.
7. Usinunue kitu ili kuonekana, au kwenda na wakati.
8. Kuwa mwaminifu, kuwa mwadilifu.
9. Timiza neno unaloahidi.
10. Sema hapana mara nyingi uwezavyo. Jambo lolote ambalo halina manufaa kwako au halitakufikisha kwneye malengo yako sema hapana.
Anza na hayo machache, halafu niandikie yale mabadiliko utakayokuwa unayaona kwa email makirita@kisimachamaarifa.co.tz
TAMKO LA LEO;
Najua hakuna mabadiliko yoyote ambayo yanaweza kutokea nje yangu. Mabadiliko yoyote ya kweli yanaanza na mimi. Kama kuna kitu chochote nataka kibadilike kwneye maisha yangu, mimi ndio wa kwanza kubadilika.
Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment