Binadamu ni viumbe wa kijamii, tunasukumwa sana kwenda kama jamii inavyokwenda. Hali hii tumeirithi kutoka kwa mababu wa mababu zetu ambao nao walikuwa mababu wa mababu zetu. Zamani ililazimika kila mtu kufanya kile ambacho kimekubalika kufanywa na jamii nzima. Hii ni kwa sababu mazingira yalikuwa hatarishi sana.
Kwa mfano kama mtu angeamua kwenda kuwinda mwenyewe badala ya kwenda na wenzake, angekuwa kwenye hatari kubwa ya kuliwa na wanyama wakali kama simba. Ili kuhakikisha watu wanakuwa na usalama, jamii nzima ilifanya mambo kwa pamoja.
SOMA; Kama Umeajiriwa Na Hujaanza Kufanya Hili Jua Kuwa Unapotea.
Sasa ni miaka mingi imepita, na hatari zile hazipo tena ila badi jamii inaishi kwneye hali ile ya kufanya mambo kwa pamoja. Naposema kufanya mambo kwa pamoja namaanisha mtu kulazimika kufanya jambo kwa sababu tu watu wengine wamefanya, hata kama halina manufaa kwake. Maisha ya sasa yamekuwa bora sana kiasi kwamba mtu anawez akuchagua kuishi anavyotaka na halazimiki kufanya kitu ambacho hapendi.
Leo nataka ujikumbushe nguvu hii muhimu unayoimiliki. Hulazimiki kufanya kitu ambacho kila mtu anafanya, hata kama jamii nzima inafanya, kama hakina manufaa kwako usifanye.Huna haja ya kuishi maisha ya unafiki ili kuwafurahisha wengine.
Changamoto nyingi kwenye maisha zinaanzia pale mtu napojilazimisha kwenda na maisha ambayo hayawezi. Kutaka kuonekana nae yupo na hivyo kuingia gharama ambazo hawezi kuzilipa.
SOMA; BIASHARA LEO; Njia Kumi Rahisi Za Kufukuza Wateja…
Fanya kile kitu ambacho unataka kweli kukifanya na unamudu kukifanya. Kinyume na hapo usijiumize na kujitengenezea changamoto.
TAMKO LA LEO;
Nakumbuka sio lazima nifanye kitu ambacho kila mtu anafanya. Nitafanya yale mambo ambayo ni muhimu kwangu na ninaweza kuyamudu. Maisha ni rahisi sana kama nitafanya kile ambacho ninapenda kufanya na nikaacha kujilinganisha na wengine.
Tukutane kwenye ukurasa wa 133 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment