Wahenga walisema mwanzo mgumu, ni kweli sio, kwamba unapotaka kuanza jambo lolote, mwanzo huwa mgumu sana. Hali hii husababisha watu wengi kushindwa kufanya mambo makubwa kwenye maisha yao.
Umeshindwa kuanza biashara ambayo umekuwa unaifikiria kwa muda mrefu. Umeshindwa kuanza kuchukua hatua ya kuboresha maisha yako yapo unajua kila hatua unayotakiwa kuchukua. Umeshindwa kuongeza thamani kwenye kazi unayoifanya. Yote hii ni sababu ya mwanzo mgumu?
SOMA; Kama Umeajiriwa Na Hujaanza Kufanya Hili Jua Kuwa Unapotea.
Lakini kwenye mwanzo huo huo mgumu kuna watu wengine wameweza kufanya mambo makubwa. Wameweza kuanza licha ya kuwepo kwa ugumu wa mwanzo. Unafikiri watu hawa ni wagumu sana kuliko ugumu wa jambo? Hapana, watu hawa ni kama wewe ila wanajua siri moja ambayo wewe huijui.
Ni siri gani wanayoijua wale wanaofanya mambo makubwa na hawazuiwi na mwanzo mgumu? Siri wanayoijua watu hawa n UGUMU WA MWANZO MGUMU. Wewe unajua kwamba mwanzo ni mgumu ila hujui ugumu wenyewe unatoka wapi. Hawa wanajua mwanzo ni mgumu na wanajua ugumu wake unatoka wapi.
SOMA; Kabla Hujabadili Tabia Zako Badili Hiki Kwanza…
Leo nakupa siri hii ya UGUMU WA MWANZO MGUMU. Ugumu wa mwanzo mgumu unatokana na mawazo yetu kuwa hasi na kuona kwamba ni vigumu kufanya jambo unalotaka kufanya. Ugumu huu unazidishwa na hadithi mbaya na ngumu kuhusu ugumu wa jambo husika. Unapokuwa unafikiria tu ugumu wa jambo, ule ugumu unaongezeka mara dufu. Inakuwa vigumu sana kwako kuanza kama kitu pekee utakachoona kwenye mawazo yako ni hali ngumu inayotokana na kujaribu kuifanya jambo hilo. Na hivyo kukupa wewe hofu ya kuanz akufanya jambo hilo.
Sasa ufanye nini? Ondoa mawazo hasi uliyonayo kwenye jambo lolote unalotaka kufanya. Tengeneza hadithi nzuri ya kufanya jambo hilo, pata picha ya mafanikio utakayokuwa nayo kw akufanya jambo hilo. Na ona hatua zote unazochukua kwenye kufanya jambo hilo ni hatua rahisi kwako kuchukua.
SOMA; SIRI YA 34 YA MAFANIKIO; Unakuwa Kile Unachofikiria.
TAMKO LA LEO;
Najua ugumu wa mwanzo mgumu unatokana na mawazo yangu hasi juu ya jambo jipya ninalopanga kufanya. Kuanzia sasa nitakuw ana mawazo chanya na nitatengeneza picha nzuri ya mafanikio nitakayofikia kwa kufanya jambo hilo. Hii itanipa hamasa ya kuanza kufanya.
Tukutane kwenye ukurasa wa 130 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment