Hakuna shaka kwamba huwezi kufikia mafanikio kama utaendelea kufanya kile ambacho unafanya sasa na kwa mtindo ambao umekuwa unautumia miaka yote. Kama utaendelea kufanya kile unachofanya utaendelea kupata matokeo unayopata.
Njia ya kupata matokeo tofauti ni kufanya mambo tofauti au kufanya mambo kwa utofauti.
SOMA; SIRI YA 34 YA MAFANIKIO; Unakuwa Kile Unachofikiria.
Njia moja ya kufanya mambo tofauti au kufanya mambo kwa utofauti ni kubadilika wewe kwanza. Yaani huwezi kupata mabadiliko kwenye maisha yako kama hutabadilika wewe kwanza.
Sasa swali ni je ili kubadilika unahitaji kufanya nini? Wengi watakimbilia kusema kubadili tabia. Ni kweli kubadili tabia kutakuwezesha kubadilisha ila mabadiliko hayo hayatadumu kama hutabadili kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiki ndio unatakiwa kukibadili kabla hujabadili tabia.
SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.
Kitu hiko ni utambulisho wako. Ndio kila mtu ana utambulisho wake, wa jinsi anavyojiona mwenyewe na watu wanavyomuona. Utambulisho wako kwako binafsi unaweza kuwa wewe ni mvivu, ni mtu usiyekamilisha mambo, ni mtu uliye na bahati mbaya, au kisirani. Hata kama utabadili tabia, kama utambulisho wako utaendelea kuwa huu, utarudi pale pale na kushindwa kufikia mafanikio.
Anza kwanza kubadili utambulisho wako, anza kujiona wewe ni mtu unayeweza kufikia mafanikio na anza kufanya kazi kulingana na utambulisho wako mpya.
TAMKO LA LEO;
Kuanzia leo nafuta utambulisho wangu wa zamani ambao hakuwa wa msingi kwangu. Sasa mimi ni mtu ambaye nafanya kazi kwa juhudi na maarifa, naweka na kusimamia malengo yangu, nakamilisha mambo niliyofanya na ni mvumilivu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 60 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment