Usitende wema kwa sababu dini inakuambia ufanye hivyo, ukitumia kigezo cha dini, kuna mazingira yanaweza kukupa nafasi ya kutokutenda wema.
Usitende wema kwa sababu unataka watu wakuone, ukitumia sababu hii utafanya mambo mabaya ukiwa kwenye kificho.
Usitende wema kwa sababu unayemtendea ni mtu unayemheshimu au kumuonea aibu, ukitumia sababu hii hutatenda wema kwa wengine.
SOMA; Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…
Tenda wema kwa sababu hayo ndio maisha uliyochagua kuishi.
Amua kwamba maisha yako yote utajaribu kadiri ya uwezo wako kuwatendea watu mema, bila ya kujali dini yako, watu wanakuonaje au ni nani unayemtendea wema. Fanya hivi kutoka ndani ya moyo wako na utapa faida kubwa sana kwa kuishi hivi.
TAMKO LA LEO;
Natenda wema kwa kila mtu ninayeklutana naye, sio kwa sababu dini inaniambia nifanye hivi, au jamii inanitegemea nifanye hivyo, au sio kwa sababu ya mtu ninayemtendea. Natenda wema kwa kila mtu kwa sababu hayo ndio maisha niliyoamua kuishi. Na sitakubali kuishi maisha yasiyoendana na msimamo wangu huu.
Tuma makala hii kwa watu watano ili tuhamasishe watu wengi zaidi kutenda wema na kujenga jamii bora.
Tukutane kwenye ukurasa wa 38 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment