Kuna wakati ambao utafanya kila unachotakiwa kufanya na kusubiri upate matokeo uliyotegemea kupata ila huyapati.
Unafanya kila kilicho ndani ya uwezo wako, unakazana sana kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa ila mwisho wa siku hupati kile ulichotarajia kupata.
Unapata kilicho tofauti kabisa, au hupati kabisa, au unaishia kupoteza kabisa.
SOMA; Mwalimu Anakusubiri, Chukua Hatua Sasa…
Ndivyo maisha yalivyo.
Unafanya kazi kwa juhudi na maarifa, unajituma sana unatoa msaada wa kutosha kwenye eneo lako la kazi ukitegemea kupewa cheo kizuri ila cha kushangaza cheo anakuja kupewa mtu mwingine.
Unaamua kufanya biashara yako kwa uaminifu mkubwa, unajituma, unakuwa mbunifu ila unaishia kupata hasara na wale unaoona wanafanya hovyo tu wanapata faida.
Katika hali hii usishangazwe au kuacha kufanya unachofanya, endelea kufanya na kuna siku mambo yatakuwa mazuri tu.
SOMA; Tunarudia Makosa Yale Yale…
Nakupa moyo, usiache kile ambacho ni sahihi kwako kufanya, endelea na siku moja dunia haitakuwa na ujanja bali kukupatia kile unachotaka.
Ila kama utakasirika na kuacha kufanya kile kizuri ulichokuwa unafanya, unaharibu nafasi zako zote za kufanikiwa baadae.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba kuna wakati nitafanya kila kilicho ndani ya uwezo wangu ila majibu yatakuja tofauti na ninavyotegemea. Sitokata tamaa wala kuacha kile ninachofanya. nitaendelea kuweka juhudi mpaka pale nitakapopata na hata nisipopata nitaendelea kufanya kile ambacho ni sahihi kwangu kufanya. Kwa sababu haya ndio maisha niliyoamua kuishi.
SOMA; NENO LA LEO; Hiki Ndio Unachohitaji Ili Kufanikiwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 58 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment