Kuna watu wana bahati eh!!
Unamuona mtu anaanza kazi, mara anapandishwa cheo na unamuona akiwa na kipato kikubwa kuliko wewe ambaye umekuwa kwenye kazi hiyo kwa muda mrefu.
Unamuona mtu anaanza biashara na baada ya muda anapata faida kubwa kuliko wewe ambaye umekuwa kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu.
Unaishia kukubali kwamba watu hawa wana bahati, na wewe huna bahati.
Usichokijua ni kwamba bahati sio kitu kinachotokea tu, bali bahati ni pale MAANDALIZI yanapokutana na FURSA. Watu hao ambao unaona wamefanikiwa kwa bahati ukweli ni kwamba walikuwa na maandalizi mapema ambayo yaliwafanya kuweza kutumia fursa zilizojitokeza mbele yao.
Hivyo kama unataka kuwa na bahati, kuwa na maandalizi mapema na fursa inapojitokeza ichangamkie mara moja.
TAMKO LA LEO;
Najua kwamba bahati ni maandalizi yaliyokutana na fursa. Nitatengeneza bahati zangu mwenyewe kwa kuwa na maandalizi ya kutosha na pale fursa inapojitokeza naitumia ipasavyo.
Tukutane kwenye ukurasa wa 40 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment