Kama umewahi kusikia hadithi moja ambapo mtu na mke wake walikuwa wanasafiri jangwani na wameoanda ngamia. Wakapishana na watu ambao walisema watu hawa wana roho mbaya sana, wanampanda ngamia mmoja watu wawili?
Waliposikia vile, mwanaume akamwambia mke wake ashuke na atembee kwa miguu, yeye akabaki amepanga. Walikutana na watu wengine waliosema, mwanaume ana roho mbaya sana, anapanda ngamia wakati mkewe anatembea kwa miguu?
SOMA; Vitu Vitamu Muhimu Unavyohitaji Ili Kuingia Kwenye Biashara.
Mwanaume akaona isiwe tabu, akamwambia mkewe apande na yeye atembee kwa miguu. Wakakutana na watu wengine waksema ona mwanaume yule alivyo bwege, anatembea kwa miguu wakati mke wake amepanda ngamia?
Mwanaume kukata mzizi wa fitina akamwambia ashuke na wote watembee kwa miguu. Walikutana na watu wengine na wakasema ona hao mabwege, wanatembea kwa miguu wakati wana ngamia, kwa nini wasimpande?
Kama ilivyo kwenye hadithi hii, huwezi kumridhisha kila mtu, watu hawataacha kusema hata ungefanya nini.
Hivyo jukumu lako ni kujua kipi unataka kufanya na kifanye kwa ubora wa hali ya juu sana. Wakati huo ziba masikio na usikubali kelele za watu zikurudishe nyuma.
TAMKO LA LEO;
Najua kwamba hata nikifanya nini lazima watu watasema. Watu watasema siwezi, wengine watasema nakosea. Lakini mimi mwenyewe ndio najua nataka nini na nitakifikiaje. Hivyo nitawekeza nguvu zangu kwenye kile ninachotaka na sitasikiliza kelele nyingine.
Tukutane kwenye ukurasa wa 36 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment