Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, February 9, 2015

UKURASA WA 40; Amua Kuwa Wewe…

Duniani kuna watu zaidi ya bilioni saba.

Lakini katika watu wote hawa, hakuna aliyefanana na wewe moja kwa moja.

Ulivyo wewe, uko wewe tu dunia nzima. Hajawahi kuwepo kama wewe na hatakuja kuwepo mwingine kama wewe.

SOMA; Fikra TANO Zinazoua Mafanikio Na Jinsi Ya Kuziepuka.

Sasa kwanini unahangaika kuwa kama wengine?

Kwa nini unalazimisha kuiga wengine? Ili ufanane nao? Ili ukubalike?

Kwa nini unajilinganisha na wengine?

Hakuna mtu mwenye uwezo wako.

Amua kuwa wewe, anza kufanya kile ambacho nafsi yako inapenda. Na kifanye vizuri sana, kiasi ambacho hakuna amewahi kufanya au hakuna atakayekuja kufanya.

Kwa kufanya hivi, kitakachotokea ni historia kwako na kwa dunia nzima. Maana utafikia mafanikio makubwa sana.

Ila kama utaendelea kukazana kuiga wengine, utaishia kuwa kawaida, na kama tunavyojua, kawaida ni sawa na hovyo.

SOMA; KAWAIDA Ni Tafsida Ya HOVYO…

NENO LA LEO;

Najua dunia nzima niko mimi kama nilivyo, hakuna mtu mwingine anayefanana na mimi kwa kila kitu. Naamua kuishi maisha yangu ili niweze kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yangu. Sitakazana kuiga au kujilinganisha mwenyewe, bali nitajilinganisha mwenyewe na malengo ninayotaka kufikia.

Tukutane kwenye ukurasa wa 40 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment