Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, February 4, 2015

#HADITHI_FUNZO; Mbinu Rahisi Iliyomwezesha Jenerali Kushinda Vita Ngumu.

Kulikuwa na mapigano makali na jeshi la Japani lilikuwa linapambana na jeshi lingine ambalo lilikuwa linaonekana kuwa na nguvu zaidi.

Generali wa jeshi la Japani aliangalia wanajeshi wake ambao walikuwa wamezidiwa namba na jeshi wanalokwenda kupambana nalo. Alikuwa na uhakika watashinda ila wanajeshi wake walionekana kujawa hofu na kukata tamaa.

SOMA; Maswali matatu muhimu ya kujiuliza leo ili kujua muelekeo wa maisha yako.

Wakati wanaelekea kupigana walipita sehemu ambayo watu huwa wanasali. Baada ya wanajeshi wote kusali, jenerali yule alitoa sarafu na kusema anarusha sarafu hiyo juu na kama itaonesha kichwa watashinda vita. Na ikiwa itaonesha mkia watashindwa vita, hii ndio itaamua hatima yetu.

Jenerali yule alirusha sarafu ile hewani na wote waliiangalia ikianguka chini na hatimaye ikaonesha kichwa. Wanajeshi wale walishangilia sana na kujawa na ujasiri na walikwend akupigana kwa ujasiri mkubwa na wakashinda.

Baada ya mapigano yale na ushindi, luteni alimfata jenerali yule na kumwambia hakuna mtu anayeweza kubadili hatima, kama imeandikwa imeandikwa. Jenerali yule alimjibu ndio na kumuonesha sarafu aliyotumia siku hiyo, ambayo ilikuwa vichwa pande zote mbili.

SOMA; NENO LA LEO; Umepangiwa Kuwa Mtu huyu…

Unajifunza nini hapa?

Kuna mambo kama matano unaweza kujifunza kwenye hadithi hii. Naanza na mawili, matatu malizia kwa kuweka maoni hapo chini;

1. Ushindi unaanzia ndani yako kwa kujiamini unaweza.

2. Unaweza kubadili hatima yako, kama utayakubali maisha yako na kuchukua hatua.

3. ________________________

4. _________________________

5. __________________________

Jaza hapo na watumie marafiki zako watano uone nao wanajifunza nini kupitia hadithi hiyo. Watumie email na wao wakutumie email.

SOMA; NENO LA LEO; Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuepuka Kupingwa.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment