Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Thursday, February 5, 2015

Kauli KUMI Za Confucius Zitakazokuhamashisha Kuboresha Maisha Yako.

Confucius alikuwa mwalimu, mwandishi, mwanafalsafa na mwanasiasa wa China. Alikuwa akiandika falsafa zinazohusu maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla.

Leo utajifunza kauli kumi kutoka kwake zitakazokuhamasisha kuchukua hatua na kuboresha maisha yako.

1. Choose a job you love and you will never have to work a day in your life.

Chagua kazi unayoipenda na hutofanya kazi tena kwenye maisha yako.

2. I hear and I forget. I see and I remember. I do and I understand.

Nikisikia nasahau. Nikiona nakumbuka. Nikifanya naelewa.

SOMA; Sheria Kumi Za Familia Za Kuzingatia

3. By three methods we may learn wisdom: first, by reflection which is noblest; second, by imitation, which is the easiest; and third, by experience, which is the bitterest.

Kwa njia tatu unaweza kujifunza hekima; kwanza kwa kutafakari ambayo ni bora; pili kwa kuiga, ambayo ni rahisi; tatu kwa uzoefu ambayo ni chungu.

4. A man who has committed a mistake and doesn't correct it is committing another mistake.

Mtu aliyefanya makosa na kutoyasahihisha anafanya makosa mengine.

5. It is man that makes truth great, not truth that makes man great.

Ni mtu anayeufanya ukweli kuwa mkuu, na sio ukweli unaomfanya mtu kuwa mkuu.

6. The will to win, the desire to succeed, the urge to reach your full potential... these are the keys that will unlock the door to personal excellence.

Utashi wa kushinda, hamu ya kufanikiwa, wito wa kufikia uwezo wako mkubwa… hizi ni funguo zitakazofungua milango ya ubora wako.

7. Real knowledge is to know the extent of one's ignorance.

Maarifa ya kweli ni kujua kiwango cha ujinga wako.

SOMA; NENO LA LEO; Uwekezaji Unaolipa Riba Kubwa Sana

8. You don't love someone for their looks, or their clothes, or for their fancy car, but because they sing a song only you can hear.

Humpendi mtu kwa muonekano wake, au nguo zake, au gari lake bali kwa sababu anaimba wombo ambao ni wewe tu unayeweza kuusikia.

9. Everything has its beauty, but not everyone sees it.

Kila kitu kina uzuri wake, lakini sio kila mtu anauona.

10. In a country well governed, poverty is something to be ashamed of. In a country badly governed, wealth is something to be ashamed of.

Kwenye nchi ambayo ina utawala mzuri, umasikini ni kitu cha aibu. Kwenye nchi ambayo ina uongozi mbovu, utajiri ni kitu cha aibu.

NYONGEZA…

11. To see the right and not to do it is cowardice.

Kuona ukweli na kutoufanya ni woga.

12. Wherever you go, go with all your heart.

Popote unapoenda, nenda na moyo wako wote.

SOMA; Njia TATU Za Kufanya Moto Wa Ujasiriamali Uendelee Kuwaka Kwenye Nafsi Yako…

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment