Tunaweza kusema matatizo yote duniani chimbuko lake ni fedha. Au kama sio yote basi sehemu kubwa ya matatizo inaanza na matatizo ya fedha.
Sina haja ya kurudia hapa kusema kwa nini fedha ni muhimu, kila mtu anajua na ndio maana tunaitafuta kwa nguvu.
Pamoja na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, kuongeza elimu na hata kulalamika na kugoma bado watu wanajikuta kwenye matatizo ya kifedha kila siku. Haijalishi umri au uzoefu, mtu aliyepo kazini mwaka mmoja na aliyepo kazini miaka kumi wote wana matatizo ya kifedha.
Hii fedha ni mdudu gani ambaye anamshinda kila mtu?
Leo tunajifunza mbinu mbili za kuondokana na matatizo ya kifedha.
Mbinu ya kwanza; tumia pungufu ya kipato chako. Yaani kama kipato chako ni laki moja basi hakikisha hutumii yote.
Mbinu ya pili; Weka akiba. Unapotumia chini ya kipato chako kile ambacho hutumii unaweka akiba, halafu unawekeza hii akiba ili iweze kukuzalishia zaidi.
SOMA; Maazimio Matano Muhimu Ya Fedha Kwa Kila Kijana Kuweka Mwaka Huu 2015.
Ni rahisi kama hivyo, lakini kwa nini watu wengi hawawezi kufanya?
Kwa sababu wanakubali kipato chao ndio kipange matumizi, yaani kipato kikiongezeka na matumizi yanaongezeka. Na pia wanasubiri watumie halafu kitakachobaki ndio waweke akiba, matumizi hayaishi.
TAMKO LA LEO;
Najua ili niweze kupata uhuru wa kifedha nahitaji kuanza kuujenga mwenyewe. Nitaujenga uhuru huu kwa kuongeza kipato changu, kuweka akiba nakuwekeza akiba hii. Kila kipato nitakachopata, sehemu fulani nitaweka akiba. Na baada ya muda akiba hii nitaiwekeza ili iweze kunizalishia zaidi.
SOMA; Njia KUMI Za Kubana Matumizi Yako Mwaka Huu 2015.
Tukutane kwenye ukurasa wa 51 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment