Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, February 3, 2015

Kauli KUMI Za Marcus Aurelius Zitakazokufanya Uyaone Maisha Kwa Utofauti.

Marcus Aurelius (26 April 121 – 17 March 180 AD)  alikuwa mfalme wa Roma kuanzia mwaka 161 mpaka mwaka 180. Alikuwa mmoja wa wafalme watano wa mwisho wa Roma ambao walikuwa na mafanikio makubwa sana. Alipitia vipindi vigumu kwenye utawala wake lakini aliweza kufanya mambo makubwa. Pia Marcus ni mmoja wa wanafalsafa wakubwa waliowahi kuishi duniani.

SOMA; Matatizo Yote Kwenye Maisha Yako Yanatokana Na Kitu Hiki.

Leo hapa utajifunza kauli kumi kutoka kwa mwanafalsafa huyu ambazo zitakufanya uyaone maisha kwa upande tofauti na kukuwezesha kufanya makubwa.

1. When you arise in the morning, think of what a precious privilege it is to be alive - to breathe, to think, to enjoy, to love.

Unapoamka asubuhi, fikiria jinsi ulivyo upendeleo wa kipekee wa wewe kuwa unaishi, kupumua, kufikiri, kufurahia, kupenda.

2. Very little is needed to make a happy life; it is all within yourself, in your way of thinking.

Unahitaji vitu vichache sana ili kuwa na maisha yenye furaha; vyote viko ndani yako, kwa jinsi unavyofikiri.

SOMA; Mambo Kumi Muhimu Kuhusu Maisha

3. Everything we hear is an opinion, not a fact. Everything we see is a perspective, not the truth.

Chochote unachosikia ni maoni, sio uhalisia. Chochote unachoona ni mtazamo, sio ukweli.

4. Accept the things to which fate binds you, and love the people with whom fate brings you together, but do so with all your heart.

Kubali vitu ambavyo vinakutokea, penda watu ambao unakutana nao, na fanya hivyo kwa moyo wako wote.

5. The happiness of your life depends upon the quality of your thoughts: therefore, guard accordingly, and take care that you entertain no notions unsuitable to virtue and reasonable nature.

Furaha ya maisha yako inategemea ubora wa mawazo yako; hivyo yalinde mawazo yako, na kuwa makini usikubali mawazo ambayo hayatakuletea furaha.

6. Waste no more time arguing about what a good man should be. Be one.

Usipoteze muda wako kubishana mtu bora anatakiwa kuwaje. Kuwa mtu huyo.

SOMA; Kitu Hiki Kimoja Kitakufanya Uweze Kujiajiri, Uishie Kuwa Mwajiriwa Au Uishie Jela.

7. The object of life is not to be on the side of the majority, but to escape finding oneself in the ranks of the insane.

Lengo la maisha sio kuwa upande wa wengi, ila kuepuka kujikuta kati ya wapumbavu.

8. He who lives in harmony with himself lives in harmony with the universe.

Mtu anayeishi kwa kuelewana na nafsi yake, anaishi kwa kuelewana na ulimwengu wote.

9. Never let the future disturb you. You will meet it, if you have to, with the same weapons of reason which today arm you against the present.

Usikubali kesho ikusumbue. Utakutana nayo kama itatokea, na utatumia silaha zilizokuwezesha kuivuka leo.

10. Life is neither good or evil, but only a place for good and evil.

Maisha sio mazuri wala sio mabaya, ila ni sehemu ya mazuri na mabaya.

SOMA; NENO LA LEO; Hapa Ndio Pa Kuanzia, Hasa kwa mwaka 2015…

NYONGEZA;

Kutokana na kauli nyingi nzuri za Marcus kuhusu maisha hapa nimeongeza nyingine mbili muhimu za kuzingatia.

We ought to do good to others as simply as a horse runs, or a bee makes honey, or a vine bears grapes season after season without thinking of the grapes it has borne.

Tunahitaji kufanya mema kwa wengine kama ambavyo farasi anakimbia, au nyuki anavyotengeneza asali, au mzabibu unavtotengeneza zabibu msimu baada ya msimu bila ya kufikiria ni zabibu gani unatoa au zitaliwa na nani.

Do every act of your life as if it were your last.
FANYA KILA UNACHOFANYA KAMA VILE NDIO KITU CHAKO CHA MWISHO KUFANYA.

Kama utaamua kupuuza vyote na kuishi kwa kauli hizo mbili za nyingeza tu, utakuwa na maisha yenye mafanikio makubwa sana.

Nakutakia kila la kheri

SOMA; Adui Yako Anaanzia Hapo Ulipo Na Anaanza hivi.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment