Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, February 10, 2015

UKURASA WA 41; Usisubiri Ukamilifu…

Moja ya kitu kinachowazuia wengi kufikia mafanikio ni kutaka UKAMILIFU.

Wanataka kuwa wakamilifu kwa kile wanachofanya.

Wanataka kila kitu kiwe tayari kabla ya kuanza.

Na wanataka wanachofanya kiwe kwa ukamilifu.

Lakini kwa bahati mbaya sana hakuna aliye mkamilifu. Hakuna wakati ambapo kila kitu kitakuwa tayari kwa ajili ya wewe kuanza kuzifanyia kazi ndoto zako. Na hata ungejiandaa vipi bado huwezi kufanya kila kitu kwa ukamilifu, lazima utakosea hapa na pale.

SOMA;  Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu; JUST DO IT.

Badala ya kusubiri uwe mkamilifu, kila kitu kiwe kamili na kutaka utoe kitu kilichokamilika, anza hapo ulipo na tumia ulichonacho. Kadiri unavyokosea ndivyo unavyojifunza. Na jinsi unavyoendelea kujifunza ndio utakaribia ukamilifu, ila huwezi kuufikia.

TAMKO LA LEO;

Najua mimi sio mkamilifu, na wala mazingira hayatakuwa kamilifu kw akila ninachotaka kufanya. Pia najua kile ninachotaka kufanya sitaweza kukifanya kwa ukamilifu. Nitaanza kufanya kwa uwezo nilionao, kwa mazingira yanayonizunguka na kadiri ninavyopitia changamoto nitaendelea kujifunza na kuboresha zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 42 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

SOMA; Sababu TATU Kwa Nini Watu Wengi Wanashinda Kufikia Mafanikio.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment