Tone la asali linavutia inzi wengi kuliko ndoo nzima iliyojaa nyongo. Unapokuwa mwema na unapofanya mema unawavutia watu wengi kuliko unavyokuwa na ubaya na kutenda mabaya. Hata kama unafanya jambo dogo kiasi gani, kama ni jema endelea kulifanya litawafikia wengi na kuwasaidia wengi pia.
Usifiche chochote kizuri ambacho unacho, usiogope kuonesha kile kizuri kilichopo ndani yako na wakati wote sukumwa kutoa kile kilicho bora. Hata kama ni kidogo kiasi gani, kitashinda ubaya ambao ni mwingi.
SOMA; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Ili Uwe Tajiri.
Weka ubora wkenye kazi ambayo unaifanya, weka ubora kwenye biashara yako, mambo madogo madogo unayofanya kila siku ndio yataongeza ubora na mwisho wa siku yatakufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Tone moja la asali litavutia inzi, sisimizi, mende, nyuki na kila aina ya kiumbe hai. Hivyo kama unataka kwenda vizuri na watu wa kila aina, kuwa tone la asali. Fanya kile kizuri unachoweza kufanya na sahau kuhusu mabaya unayoweza kufanya.
Kizuri kidogo ni bora kuliko kibaya kikubwa. Kama mtu anakufanyia ubaya wewe mfanyie wema na usibabaike. Mwisho wa siku wema utavuta vizuri zaidi kuliko ubaya.
TAMKO LA LEO;
Najua tone moja la asali litavutia vitu vingi kuliko ndoo nzima ya nyongo. Nitahakikisha maisha yangu yanakuwa tone la asali kwa wengine. Nitafanya ubora kwenye kazi/biashara yangu na nitatenda mema kwa watu wote. Hii ndio njia ya uhakika kwangu kufikia mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 125 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment