Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, May 11, 2015

UKURASA WA 131; Njia Rahisi Ya Wewe Kuondokana Na Tabia Usiyoipenda.

Watu wengi sana huwa wanaweka malengo ya kubadili maisha yao lakini wanashindwa kufikia malengo hayo. Na ili mtu uweze kubadili maisha yako unahitaji kuanza na kubadili tabia zako kwanza. Kubadili tabia kumekuwa ni kugumu sana na ndio maana watu wengi hujikuta pale pale walipokuwa miaka mingi iliyopita.

Sikiliza hivyo ulivyo leo, ndivyo utakavyokuwa miaka mitano ijayo, tofauti ni watu utakaokutana nao na vitabu utakavyosoma. Sasa kama utasoma vitabu kuna nafasi unaweza kubadilika. Kama hutasoma kabisa ndio utazidi kuwa umerudi nyuma.

SOMA; Hivi Ndivyo Utakoweza Kuishi Na Mtu Wa Aina Yoyote Ile Kwa Furaha Na Amani

Sasa kwa nini kubadili tabia kumekuwa kugumu sana? Kwa nini huwezi kuacha kunywa pombe licha ya kujaribu kufanya hivyo mara nyingi? Kwa nini huwezi kuacha kula vyakula vya hovyo? Kwa nini huwezi kuacha kupoteza muda? Japokuwa umekuwa na nia ya dhati ya kufanya mambo haya unaishia kukwama.

Leo nakushirikisha njia moja rahisi sana ya kukuwezesha kuondokana na tabia yoyote hata kama ni sugu kiasi gani.

Njia hiyo ni kujipa picha ya jambo baya sana ambalo litatokea kama wewe hutobadili tabia uliyonayo sasa. Na weka picha hii kwenye akili yako pale ambapo unataka kufanya tabia hiyo. Kwa mfano kabla hujanywa pombe, jipe picha ya matatizo makuwba ya kiafya utakayokuwa nayo kwa sababu ya kuendekeza pombe. Ona upo kwenye kitanda cha hospitali ukiwa hujiwezi kwa sababu ya pombe ambazo umekuwa unakunywa kw amuda mrefu.

SOMA; Fanya Uwekezaji Huu Ambao Ni Rahisi Kwako Na Una Faida Kubwa.

Kama unataka kufanya jambo ambalo litakupotezea muda, jipe picha ya jinsi muda utakaopoteza leo utayafanya maisha yako yaendelee kuwa magumu. Ona jinsi ambavyo utakuwa na kazi ya hovyo au biashara yenye hasara na inayokutesa kwa sababu tu leo hukutumia muda wako vizuri.

Kwa kujijengea picha za aina hii utajiondolea ila hamasa inayokusukuma kufanya tabia fulani na hivyo kuacha kufanya tabia hiyo.

TAMKO LA LEO;

Sitafanya jambo lolote ambalo kwa miaka mingi ijayo litaniletea matatizo makubwa. Nitajipa picha ya hali mbaya itakayotokea kwa mimi kushindwa kubadili tabia yangu leo.

Tukutane kwenye ukurasa wa 132 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment