Katika dunia tunayoishi, kuna
makundi mawili ya watu. Kuna kundi la watu ambao ni wazalishaji, hawa ni watu
ambao wanatuletea vitu vyote tunavyotumia. Simu, tv, vyakula vizuri, vitabu,
makala tunazosoma, nguo tunazovaa, magari na vingine vingi. Kundi la pili ni la
watumiaji. Hawa ni watu ambao wanatumia vitu hivi vinavyotolewa na wazalishaji.
Kwanza kabisa kila mmoja wetu
ni mtumiaji wa kitu kinachotengenezwa na wengine. Huu sio ulimwengu ambao
unaweza kujitegemea wewe mwenyewe kwa kila kitu. Unategemea vitu vingi sana
kutoka kwa wengine ili maisha yako yaweze kwenda vizuri.
Swali kubwa la kujiuliza ni
je wewe unazalisha nini? Ndio umekuwa mtumiaji mzuri, lakini ni kitu gani
ambacho unazalisha kwa ajili ya wengine? Unatumia simu nzuri na kuifurahia ila
kumbuka kuna mtu amekaa chini, usiku na mchana kutengeneza simu hiyo nzuri
unayoipenda leo. Je wewe ni kitu gani kimekuchukua usiku na mchana kufanya na
kikafika kwenye mikono ya watumiaji wakafurahi sana? Unavaa nguo nzuri na
kujiona unakwenda na wakati, umependeza, lakini kuna watu ambao wamefanya kazi
kubwa sana mpaka wakaweza kuja na nguo hizo.
Kazi yako au biashara yako
ilikuwa iwe sehemu nzuri sana ya wewe kuzalisha, lakini je unazalisha kupitia
hiko unachofanya? Ni kweli unahangaika usiku na mchana kuhakikisha kile
unachozalisha kikimfikia mtu atakifurahia sana? Je unatoa kile kilicho bora
sana na kujisukuma zaidi ili kufanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi? Kama ambavyo
wengine wanafanya kwenye maisha yako?
Wakati mwingine unapoangalia
kitu kizuri unachotumia, jiulize ni kitu gani wewe umezalisha na mtu anayekitumia
anafurahia kama wewe unavyofurahia kilichozalishwa na wengine. Hii ikupe hasira
ya wewe kuzalisha kilicho bora zaidi. Usikubali kuwa mtumiaji tu, kuwa
mzalishaji pia.
TAMKO LA LEO;Nimechoka kuwa mtumiaji na kufurahia vitu vilivyozalishwa na wengine tu. Sasa na mimi nitakuwa mzalishaji ambaye natoa vitu wengine watavifurahia na kuboresha maisha yao. Nitafanya hivi kupitia kazi au biashara ninayofanya. Najua sijayaishi maisha yangu kama sijaweza kuyabadili maisha ya mwingine kupitia ninachofanya.
Tukutane kwenye ukurasa wa 152 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee
kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa
ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment