Tunaishi dunia ambayo kila mtu kuna kitu anatafuta. Na kipimo kimoja ambacho kinapima kile ambacho kila mtu anataka ni fedha. Kama unataka kuwa na maisha yenye hadhi nzuri basi yatapimwa kwa kiwango cha fedha unachotengeneza au ulichonacho. Hivyo kwa kila wakati kila mmoja wetu anapambana kupata fedha. Tunafanya kazi na biashara zinazowasaidia wengine ila mwisho wa siku tunataka na sisi kupata fedha ambazo zitatusaidia kwatika mahitaji mengine muhimu.
Katika mchakato huu wa maisha
wa kila mtu kutafuta fedha, imefika hatua sasa kila mtu anawinda fedha
uliyonayo wewe. Kila mtu anakazana kukushawishi utoe fedha yako ili aipate
yeye. Mtu anayeuza nguzo nzuri na kukushawishi kwamba huwezi kupata nyingine kama
hizo anafanya yote hayo ili aipate fedha uliyonayo mfukoni. Mtu anayeandaa
tamasha na kukuambia kwamba ni la kukata na shoka, hutakiwi kulikosa, anatumia
mbinu zote hizo kuhakikisha wewe unatoa fedha yako na yeye anufaike kwa kiasi
chake.
Jua kwamba kila mtu
unayekutana naye katika mazingira ya kazi au biashara anatafuta jinsi ya
kuipata fedha yako. Sio jambo baya kwa kuwa unapata huduma, ila pia kuna somo
kubwa sana unatakiwa kujifunza hapa. Kama kila mtu anaiwinda fedha yako, je
wewe ni juhudi gani unazofanya kuilinda isichukuliwe hovyo?
Huwezi tu kutoa fedha kwa
sababu mtu amekushawishi ufanye hivyo, japo kuna wengi wanafanya hivi,
unakutana na muuza nguo, hukuwa na mpango wa kununua nguo ila unajishangaa
umenunua na unafika nyumbani nguo yenyewe hujaipenda. Ni lazima wewe uwe na
ulinzi mkubwa kwenye fedha zako, la sivyo utajikuta unampatia kila mtu na wewe
mwenyewe unabaki mikono mitupu.
Kuwa mlinzi imara wa fedha
zako, hakikisha unatumia kwenye matumizi ambayo ni muhimu sana. Kesho
nitakushirikisha njia nyingine muhimu ya kuzilinda fedha zako na pia
kuhakikisha na wewe unaziwinda fedha zako mwenyewe. Mshirikishe watu wako wa
karibu ujumbe huu kwa kuwatumia email, ni muhimu sana wewe kufanya hivi kwa
sababu karibu kila mtu ana matatizo ya fedha, na matatizo yote ya fedha
yanaanzia hapa kwenye uwindaji. Mshirikishe mtu na utakuwa umefanya jambo zuri
sana.
TAMKO LA LEO;Najua kila mtu anawinda fedha ambayo ipo kwenye mfuko wangu. Kila mtu anayenishawishi kununua kitu anawinda fedha zangu. Ni jukumu langu kuweka ulinzi kwenye fedha zangu ili na mimi niweze kunufaika nazo.
Tukutane kwenye ukurasa wa 153 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee
kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa
ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke
email.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya
facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment