Moja ya sababu ambazo watu wamekuwa wakizitumia kwamba zinawazuia kufikia mafanikio ni kutokujua vitu fulani au kwa kuelewa zaidi kutokuwa na uzoefu. Kwa kuwa mimi lengo langu ni kukuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa, nahakikisha visababu hivi vinakosa nguvu na wewe unaanza kufanyia kazi kile unachotaka kupata.
Sasa leo tuanze na vitu ambavyo huvijui. Kama kuna vitu hujui, kama kuna vitu huna uzoefu navyo, kwanza hongera sana kwa sababu umedhibitisha kwamba wewe ni binadamu. Kila mtu alizaliwa akiwa anajua kitu kimoja kikubwa, jinsi ya ku “survive”, yaani jinsi ya kupona kwenye haya mazingira. Ndio maana mtoto hata akizaliwa leo, anajua kunyonya na kulia pia ili kufikisha ujumbe kwamba kuna kitu sio kizuri.
Lakini vitu vingine vyote kwenye maisha yako, ulizaliwa ukiwa hujui na sasa unajua. Je kuna maajabu hapa, la hasha, ulijifunza. Ulizaliwa hujui kusoma wala kuandika, ila sasa hivi upo hapa na unasoma makala hizi nzuri zinazokupatia maarifa. Ulizaliwa ukiwa hujui lugha yoyote zaidi ya kulia, la kwa sasa huenda unajua lugha sio chini ya tatu. Ulizaliwa ukiwa hujui kupika, kuendesha chombo cha usafiri na vingine vingi ambavyo kwa sasa unafanya, lakini uliweza kujifunza na sasa unavifanya.
Sasa kwa nini unatumia hicho unachoshindwa kufanya sasa kama kigezo cha wewe kuacha kufanya au kama sababu ya kushindwa? Si unaweza kujifunza kama ulivyojifunza hivyo vitu vingine?
SOMA; Umuhimu Na Jinsi Ya Kujenga Uaminifu Kwa Wateja Wako.
Kama kuna kitu chochote ambacho unafikiri kwa kutokukijua kinakuzuia kufikia mafanikio, jifunze kitu hicho. Tunaishi kwenye dunia ambayo kujifunza kumerahisishwa sana. Kwa kutumia simu yao tu unaweza kujifunza chochote unachotaka kujifunza. Tumia nafasi hii vizuri. Iwe unataka kujifunza upishi, iwe kujifunza uandishi, iwe kujifunza lugha ya kigeni, iwe kujifunza biashara na mengine mengi yanawezekana.
Wakati mwingine ukisema kwamba hujafikia mafanikio uliyotaka kwa sababu hujui kitu fulani utakuwa unatudanganya, maana ukweli ni kwamba ulikuwa na nafasi ya kujua ila hukuitumia vizuri. Anza sasa kuitumia nafasi hiyo.
TAMKO LA LEO;Tukutane kwenye ukurasa wa 166 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kitu chochote ambacho sikijui sio kikwazo kwangu kufikia mafanikio, bali hiki ni kitu muhimu ninachotakiwa kujifunza ili niweze kufikia mafanikio makubwa. Nitajifunza kila kitu muhimu ninachotakiwa kujua ili kufikia mafanikio, kama ambavyo nimejifunza vitu vingine kwenye maisha.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment