Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, June 2, 2015

UKURASA WA 153; Huyu Ndio Pekee Anayefanana Na Wewe Kwa Kila Kitu.


Katika dunia hii ambayo ina watu zaidi ya bilioni saba, kuna mtu mmoja tu ambaye anafanana na wewe kwa kila kitu. Hii ni kuanzia uwezo, ubunifu, vipaji na hata mipango mbalimbali ya kimaisha. Kwa kumjua mtu huyu na kushirikiana naye vizuri kutakuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa sana.
Utafikia mafanikio makubwa kwa kumjua mtu huyu kwa sababu utaacha kuwaiga wengine na kumuiga huyu ambaye unafanana naye kwa kila kitu. Kinachokurudisha nyuma ni kuiga wengine ambao hamfanani hata kidogo. Unaiga watu ambao wana uwezo tofauti na wako, wana vipaji tofauti kabisa na hata mipango yao ya maisha ni tofauti na ya kwako. Hivyo unavyokazana kuwa kama wao unashangaa huna furaha wakati wao unawaona wana furaha muda wote.
Sasa umefika wakati wa wewe kumjua yule ambaye unafanana naye kwa kila kitu ili uanze kumuiga mtu sahihi kwako. Na kumuiga mtu huyu utakuwa na uhakika wa kufanya mambo makubwa sana kwenye maisha yako.
Mtu pekee kwenye dunia hii ambaye unafanana naye kwa kila kitu ni WEWE MWENYEWE. Wewe mwenyewe ndio uko hivyo katika watu zaidi ya bilioni saba duniani. Hata kama mmezaliwa mapacha wa kufanana, bado hamfanani kwa kila kitu. Kila mmoja ana utofauti wake katika maisha ambao unamfanya awe yeye. Upo wewe tu hapa duniani na hakuna mwingine kama wewe.
Hivyo usijaribu kumuiga mtu yeyote, kila mmoja wetu ana utofauti wake. Usijaribu kushindana na wengine, wewe tayari ni mshindi kwa upande wako. Kikubwa unachotakiwa kufanya ni kuweka juhudi kufikia uwezo mkubwa ambao uko ndani yako. Nimesahau kukuambia kwamba pamoja na wewe kuwa tofauti na wengine wote, bado una uwezo mkubwa sana kwenye vitu fulani ambapo duniani hakuna mwenye uwezo kama wako. Jua vitu hivi na ishangaze dunia.
Kila mmoja wetu anayo nafasi ya kuishangaza dunia kwa kufanya kitu ambacho hakikuwahi kufanya na mtu mwingine yeyote. Usikubali kuondoka hapa duniani kimyakimya bila ya kuishangaza dunia na kuacha alama.
Wewe ndiye mtu pekee unayefanana na wewe. Acha wengine wafanye yale ambayo wanaweza kuyafanya kwa ubora na wewe fanya kile unachoweza kufanya kwa ubora.

TAMKO LA LEO;
Najua katika dunia yenye watu zaidi ya bilioni saba, hakuna hata mmoja anayefanana na mimi kwa kila kitu. Mimi ni wa pekee na nina uwezo mkubwa sana. Nikiweza kutumia huu uwezo wangu kutaishangaza dunia na kuacha alama kwenye maisha ya wengine. Naanza kufanyia uwezo wangu kazi na ni lazima niishangaze dunia, lazima niache alama kwneye maisha ya wengine.

Tukutane kwenye ukurasa wa 154 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment