Watu wanaofanya
kwenye idara ya zima moto kazi yao ni moja tu, kusubiri moto utokee na kwenda
kuuzima. Kama hakuna moto, hawana kazi kubwa, ila moto unapotokea ndipo hufanya
kila juhudi kuuzima.
Sasa kuna
watu wengi kati yetu ambao wanaishi maisha ya zima moto. Watu hawa wanaweza
kuwa na malengo na mipango mizuri ila wanashindwa kuitekeleza kwa sababu ya
mtindo wa maisha waliochagua kuishi ambao ni wa kuzima moto. Watu hawa
huhangaika kuzima kila moto ambao unajitokeza kwenye maisha yao.
Watu hawa
huishi siku yao kutokana na kitu kilichotokea. Husumbuka na kila kitu kinachotokea
hivyo kushindwa kufanyia kazi malengo waliyojiwekea. Na mara nyingi moto
wanaozima hauhusiani kabisa na malengo yao hivyo kujikuta wakizidi kupoteza
muda.
Kuna uwezekano
mkubwa na wewe ni mmoja wa wanaoishi kwa kuzima moto. Ngoja nikupe sifa za
wanaozima moto uone kama sio mmoja wao. Kama huwezi kutenga muda wa kufanya
kuondokana na kelele nyingine zote wewe ni zima moto. Kama huwezi kukaa mbali
na simu yako kwa muda ambao unahitaji kufanya kazi wewe ni zimamoto. Kama unajibu
haraka kila ujumbe unaoingia kwenye simu yako, au kuperuzi mitandao ya kijamii
ukifikiri kuna kitu kinakupita, wewe ni zimamoto.
Kama wewe
umeingia kwenye kundi la zima moto, nina habari mbili kwako, moja nzuri na moja
mbaya. Naanza na habari mbaya, hutaweza kufikia mafanikio kwenye maisha kwa
kuwa zima moto. Na habari nzuri ni kwamba unaweza kubadili tabia hiyo ya zima
moto. Ni wewe kujijengea nidhamu ya kuweza kusimamia mipango yako na kuachana
na mambo yasiyokuwa muhimu kwako. Ni vigumu lakini inawezekana. Kama unahitaji
msaada wa kuweza kuondokana na tabia ya zima moto tuwasiliane.
TAMKO LA LEO;Najua kwa maisha ya kuzima moto ninayoenda nayo, sitaweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yangu. Naamua sasa kuishi kwa kufuata malengo na mipango yangu na sio kutafuta moto wa kuzima. Moto wangu ni malengo na mipango yangu, vingine vyote ni kelele tu.
Tukutane kwenye
ukurasa wa 158 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi
mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe
wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia
watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili
kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment