Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, June 26, 2015

UKURASA WA 177; Ndio, Kwa Hiyo...

Ni vigumu sana kuweza kufanikiwa kwenye biashara, ndio kwa hiyo unahitaji kujipanga vizuri na kutokukata tamaa ili uweze kufikia mafanikio unayotarajia.
Umri wangu ni mdogo/mkubwa sana kuweza kuanza kufanya jambo hili sasa. Ndio kwa hiyo unahitaji kuwa wa tofauti, licha ya umri wako kuwa usiotegemewa bado unaweza kuweka juhudi na ukafikia kile ambacho unataka.
Nimejaribu mara nyingi sana lakini nimeshindwa. Ndio kwa hiyo unahitaji kubadili mbinu zako, kuendelea kufanya kitu kile kile na kutegemea majibu tofauti ni ujinga wa kupindukia.
Napenda sana kuanza biashara ila sina mtaji. Ndio kwa hiyo unahitaji kufikiria njia ya kuweza kuanza biashara kidogo au kutafuta kitu kingine cha kukuingizia kipato kwa sasa ili ujiandae na kuingia kwenye biashara unaotazamia.
SOMA; Vitu Ambavyo Ni Rahisi Kufanya.... Na Madhara Yake.
Ukweli ni kwamba mtu yeyote anaweza kuja na sababu zaidi ya elfu moja kwa nini hawezi kufanya kitu fulani. Ila sababu hizi haziwezi kusaidia chochote.
Watu waliofanikiwa wanakuja na sababu lakini huzipatia sababu zao suluhisho ambalo hulifanyia kazi na hatimaye kufanikiwa.
Usiwe mtu wa kutafuta au kutoa sababu tu. Hebu anza kuzipa sababu zako suluhisho na utaona fursa nyingi sana za kukufikisha kwenye kile unachotaka.
Wakati wowote unapokuja na sababu tafadhali sana mbele yake ongeza NDIO KWA HIYO....
TAMKO LA LEO;
Najua sababu yoyote ninayojipa haiwezi kunifikisha kule ninakotaka kwenda. Ila ninapoifanyia kazi sababu ninayoipata ndio natoa nafasi kubwa kwangu kuweza kupata kile ninachotaka. Najua mjinga yeyote anaweza kuja na sababu kwa nini hafanikiwi na hii ndio inazidi kumfanya asifanikiwe. Lakini mimi sio mmoja wa wajinga hawa, kila sababu ninayopata lazima niipatie ufumbuzi.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment