Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Friday, June 12, 2015

UKURASA WA 163; Unapokuwa Mpinzani Wako Mwenyewe... Na Hasara Yake Kwenye Maisha Yako.


Moja ya changamoto kubwa zinazowazuia watu wengi kupata kile wanachotaka, kufikia mafanikio wanayotarajia ni kuwa wapinzani wao wenyewe. Yaani wewe unakuwa mpinzani wako mwenyewe. Bado hujaelewa inakuwaje? Nitakufafanulia vizuri zaidi ili uweze kuelewa na kuchukua hatua pia.
Umekuwa unajifunza mambo mazuri na yatakayobadili maisha yako na unakubali kabisa ya kwamba utakwenda kufanyia kazi yale ambayo umejifunza. Ila unapoanza kuyafanyia kazi yale uliyojifunza yanaanza kukujia mawazo kwamba unachofanya sio sahihi au hakiwezi kukuletea kile unachotaka.
Labda umejifunza kuhusu kuamka asubuhi na mapema ili ufanye mambo yako ukiwa na utulivu. Unaamka siku ya kwanza na ya pili baada unaanza kufikiria kwa nini nijitese, au ina maana gani, acha niendelee na muda wangu wa kawaida wa kuamka.
Au umejifunza kutolalamika au kulaumu mtu yeyote yule, iwe ndugu, serikali, bosi, bali wewe ni kuchukua hatua. Baadae unaona haiwezekani, hawa watu ni lazima walaumiwe, wanafanya mambo ambayo sio. Unawalaumu, unaridhika na maisha yako yanaendelea kuwa kama yalivyokuwa zamani.
SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.
Leo nikuambie kitu kimoja kwamba kuwa adui yako mwenyewe ni kikwazo namba moja kwako kubadili maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. Unaweza kuwa na mawazo mazuri sana, unaweza kuwa na mipango mizuri sana ila kama hutaacha kuwa adui yako mwenyewe, kama hutaacha kuwa mpinzani wako mwenyewe hakuna kitakachobadilika kwenye maisha yako.
Safari ya kubadili maisha yako na kufikia mafanikio sio rahisi kama unavyofikiri. Utapata upinzani mkubwa kuanzia ndani yako mwenyewe na hata kwa wale wanaokuzunguka. Ukishafanya maamuzi ya kubadili maisha yako, komaa nayo na usirudi tena nyuma, hata kama utajipa sababu nzuri kiasi gani.
TAMKO LA LEO;
Najua mara nyingi nimekuwa mpinzani wangu mwenyewe. Nimekuwa napanga kubadili maisha yangu ili kufikia mafanikio lakini mimi mwenyewe naanza kupinga vile nilivyopanga kufanya. Kuanzia leo naondoa kabisa upinzani mkubwa ambao nimekuwa najiwekea mwenyewe. Nikishapanga kitu nitakomaa nacho mpaka mwisho, mpaka nione kile ninachotarajia kuona.
Tukutane kwenye ukurasa wa 164 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment