Tumewahi kujadili hapa kwamba
matatizo uliyonayo umeyatengeneza wewe mwenyewe. Hii inatokea kwa sababu kwa kila
tatizo ulilonalo, unapojaribu kulitatua unatengeneza tatizo jingine. Kila suluhisho
linakuja na tatizo jipya kabisa. Hivyo unaweza kuchagua ni matatizo ya aina
gani unafanya.
Kuna wakati mtu anaweza kuwa
kwenye matatizo makubwa sana na akawa hajui afanye nini. Ila anapokuambia wewe
kuhusu matatizo yake unaona suluhisho haraka sana na kushangaa kwa nini mtu
huyu haoni suluhisho hilo rahisi. Hii yote inatokana na sababu moja kubwa
ambayo inawafanya watu washindwe kutatua matatizo yao, japo suluhisho ni
rahisi.
SOMA; Kila Mtu Anawinda Kitu Hiki Muhimu Ulichonacho, Kuwa Makini.
Sababu moja kubwa
inayokufanya wewe ushindwe kutatua matatizo yako ni kutokukua zaidi ya matatizo
yako. Kama tulivyoona hapo juu matatizo uliyonayo umeyatengeneza wewe mwenyewe.
Na umeyatengeneza matatizo haya ukiwa na uwezo mzuri sana wa kufikiria. Hivyo kwa
kuendelea kufikiria kama ulivyokuwa unafikiria wakati unatengeneza matatizo
hayo huwezi kuyatatua kamwe. Unahitaji kuweza kufikiria zaidi ya ulivyokuwa
ukifikiria wakati unaingia kwenye matatizo yako.
Unahitaji kuwa mbunifu zaidi
ya ulivyokuwa wakati unatengeneza matatizo yako. Kwa kifupi kuwa vile
ulivyokuwa wakati unaingia kwenye matatizo hakuwezi kukusaidia hata kidogo
kutatua matatizo hayo. Unahitaji kuwa mtu tofauti na ulivyokuwa mwanzo,
unahitaji kuweza kufikiri zaidi na kuwa mbunifu zaidi ya wakati unaingia kwenye
matatizo hayo.
Unaweza kufikiria zaidi ya
ulivyokuwa unafikiri wakati unaingia kwenye matatizo na unaweza kuwa mbunifu zaidi
ya ulivyokuwa wakati unaingia kwenye matatizo kama utakuwa matu wa kujifunza kila
siku kwa kujisomea na kutafakari. Pia unahitaji kuilazimisha akili yako
kufikiri zaidi na kutengeneza majibu ya changamoto unazopitia.
TAMKO LA LEO;Najua siwezi kutatua matatizo niliyonayo kama nitaendelea kufikiria kama nilivyokuwa nafikiria wakati naingia kwenye matatizo haya. Nahitaji kuwa na mabadiliko ya kifikra na kiutendaji ili kuweza kukabiliana na matatizo ninayokutana nayo. Nahitaji kuwa mbunifu zaidi ya nilivyokuwa wakati naingia kwenye matatizo haya.
Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo
mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook
au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment