Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, June 9, 2015

UKURASA WA 160; Poteza Vitu Vyote Ila Sio Hiki Kimoja Muhimu.



Unaweza ukapoteza vitu vyote kwenye maisha yako, ndio namaanisha vyote. Iwe ni magari, nyumba, fedha zenyewe na kila kitu cha thamani ambacho umetumia nguvu nyingi kukipaya kwenye maisha yako. Ila utaweza kuvipata vyote kama hutapoteza kitu kimoja muhimu sana. Kitu hiko utajifunza leo hapa baada ya muda mfupi.
Kabla hujajifunza kitu hiko, nikuambie kwamba kama wewe sio mwizi au fisadi na umeweka juhudi na maarifa kupata kile ambacho umekipata, basi una uwezo wa kupata vingine vingi zaidi ya ulivyonavyo sasa. Hii ni kwa sababu wewe una uwezo wa kutengeneza kipato. Wewe una kitu fulani ambacho ukikifanya, watu wanakuwa tayari kukupa wewe fedha. Iwe ni kazi au biashara au hata kipaji fulani unachotumia, lakini watu wanakuwa tayari kukulipa wewe kwa kile unachofanya.
Tunaita kitu hiki uwezo wa kutengeneza kipato na ndio kitu unachotakiwa kukilinda kwenye maisha yako. Poteza kila kitu kwenye maisha yako, lakini usipoteze uwezo wako wa kutengeneza kipato. Maana ukishapoteza uwezo huu, na wewe umepotea. Ila utakapoendelea kuwa na uwezo huu, hata kama utapoteza vitu vingine vingi ulivyonavyo utaweza kuvirudisha.
Kuna faida nyingine kubwa ya kujua uwezo wako wa kutengeneza kipato, hii itakuletea uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako. Kuna watu ambao wanafikiri wameajiriwa kwa huruma tu, na hivyo kuogopa kupoteza ajira zao kwa sababu hawatapata ajira nyingine au kipato kingine. Hii sio kweli kabisa, japo waajiri wanataka wewe uamini hivyo. Kama ungekuwa umeajiriwa kwa huruma ungeshafukuzwa zamani sana, kuna thamani ambayo unaitoa na ndio maana unalipwa. Jua thamani hii na iboreshe zaidi, hata ukiamua kuondoka kwenye ajira hiyo unajua uwezo wako wa kutengeneza kipato bado unao.
Unawezaje kujenga uwezo huu wa kutengeneza kipato? Kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo unajifunza. Na kitu cha kwanza ninachokushauri ufanye, kama bado hujafanya, soma kitabu JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA. Hapa utaweza kujua mabadiliko muhimu kwenye kazi au biashara yako na hivyo kuendelea kukuza kipato chako zaidi. Kama hujasoma kitabu hiki kisome sasa, kama huna mpango wa kukisoma umeamua mwenyewe kukataa uhuru wako.
TAMKO LA LEO;
Hata kama nitapoteza kila kitu, nitalinda kitu kimoja muhimu sana, kitu hiki ni uwezo wangu wa kutengeneza kipato. Hii ndio silaha yangu kubwa itakayoniwezesha kushinda kwenye ulimwengu huu ambao una changamoto nyingi. Nitaendelea kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo najifunza ili nikuze na kuimarisha uwezo wangu wa kutengeneza kipato. Najua nikipoteza uwezo huu ndio nimepoteza kila kitu kwenye maisha yangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 135 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment