Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, June 23, 2015

UKURASA WA 174; Je Unafanya Kile Unachopenda Au Unachotegemewa Kufanya?(Na Mbinu Za Kuweza Kufanya Kile Unachopenda Kufanya)

Ni jambo la kushangaza kwenye maisha kwamba baadhi yetu tunaishi maisha ambao hata hatuyajui. Tunatumia muda wetu mwingi kuishi maisha ambayo hata hatukupanga kuyaishi. Tunajikuta tunaishi maisha tofauti kabisa kwa sababu tunalazimika kuishi maisha ambao kila mtu anaishi.
Tumeshazungumza sana kuhusu kuishi maisha ya wengine, leo ngoja tuzungumze kufanya kazi za wengine.
Kama imetokea kazi unayoifanya ikawa ndio kitu unachopenda kufanya upo kwenye nafasi nzuri sana. Na mafanikio yapo mbele yako. Ila ni nadra sana kuwa kwenye kundi hili ambalo lina watu wachache, asilimia 3 tu ya watu kwenye jamii.
Kama upo kwenye asilimia 97 iliyobaki, maana yake unafanya kazi unayofanya kwa sababu tu ndio unayotegemewa kufanya. Unafanya kwa sababu unafikiri ndio njia pekee ya kukupatia wewe kipato. Na kila mtu ameshakuaminisha hivyo na huwezi kuona nafasi ya kuondoka kwenye hilo.
SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Kinaitwa SELF-IMPROVEMENT 101.
Kama unafanya kile ambacho kila mtu anakutegemea ufanye, leo nataka nikupe mbinu ya kuanza kufanya kile ambacho unapenda kufanya.
Kwanza kabisa jua ni kitu gani unapenda, licha ya kazi ambayo sasa unaifanya. Amua ni kipi unapenda kukifanya na kila ukikifanya unajisikia vizuri sana. Iwe ni sanaa, iwe ni kitu cha kuwasaidia wengine, iwe ni mchezo na kadhalika. Chochote kile kinachokufanya ujisikie vizuri ni kitu muhimu sana kwako.
Baada ya kujua kitu hiki panga ni vipi unaanza kukifanya. Jua kwa sasa upo wapi na utaanzia wapi ili kufika wapi.
Kisha tenga muda kila siku wa kufanya kitu hiki. Kama kinahusiana na biashara, tenga muda kila siku wa kufanya biashara hiyo. Huna haja ya kuanzia mbali, anza kidogo na anza kwa kutafuta mteja mmoja, mpatie bidhaa au huduma nzuri na hakikisha unabadili maisha yake kupitia kile unachofanya. Tafuta tena mteja mwingine na fanya kama ulivyofanya kwa mteja wa kwanza na endelea kuboresha. Wakati huu bado unaendelea na kazi yako hivyo hujali sana kuhusu kipato, bali kutoa kitu bora ambacho kitawafanya wengine wakuzungumzie.
Ukiendelea hivi kwa muda, miaka kadhaa utafikia kuwa na wateja wengi kiasi kwamba kipato unachopata kwenye ajira yako ni kidogo ukilinganisha na hiki cha pembeni. Na hapo unakosa muda wa kuwahudumia wateja wako wote. Hapa ndio unaacha kazi na kufanyia kazi kitu hiko moja kwa moja.
Uko makini na umejitoa kutengeneza kitu kama hiki na unahitaji muongozo zaidi? Tuwasiliane, niandikie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz na niambie ni nini unataka kufanya na tutajadili jinsi ya kuweza kupata muongozo mzuri. Ukiwa mwenyewe ni rahisi kukata tamaa, ukiwa na mwongozo utapata hamasa ya kwenda zaidi.
TAMKO LA LEO;
Najua ninachofanya sasa sio kile ambacho napenda kufanya bali ambacho kila mtu anategemea nifanye, ili nipate kipato cha kuendesha maisha. Sasa nimeamua kutenga muda kila siku na kuanza kufanyia kazi kile ambacho ninapenda kufanya. Nitaweka juhudi kubwa kwenye kitu hiki na najua kwa muda wa mbeleni kitakuwa chanzo changu kikubwa cha mapato.
Tukutane kwenye ukurasa wa 175 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment