Kuna mambo mengi
sana unayohitaji kufanya na unayoweza kufanya kwenye maisha yako. Lakini sio
mambo yote unayotaka kufanya ni muhimu kwako au yatakufikisha kwenye malengo
uliyojiwekea. Hivyo ni muhimu sana kujua ni kitu gani unafanya na kina umuhimu
gani.
Hakuna kitu
kinauma kama kufanya vizuri sana kitu ambacho hakikutakiwa kufanywa kabisa. Au kufanya
vizuri kitu ambacho sio muhimu huku kuna vitu muhimu ambavyo hujavifanya.
Kwa mfano
unakwenda kwenye kazi yako asubuhi, kabla hujatimiza majukumu yako ya kikazi
unahakikisha unajibu meseji zote ambazo watu wamekutumia, unajibu email zako
zote na kuangalia facebook kama kuna mtu kakutaja au kuchangia kwenye kitu
ulichoandika. Utakamilisha vizuri mambo haya lakini yanachangia kiasi gani
kwenye mafanikio yako. SIFURI!!
Kabla
hujaanza kufanya jambo lolote, jiulize je hili ni jambo muhimu sana kwako kuweza
kufikia mafanikio unayotarajia? Kama jibu ni hapana, jiulize tena; je mambo
yote muhimu niliyopanga kufanya leo nimeshayakamilisha? Kama jibu ni ndio
endelea na hiko unataka kufanya. Kama jibu ni hapana, acha mara moja na nenda
ukatekeleze kile ambacho ni muhimu kwanza.
Usifanye kitu
ambacho sio muhimu kama una kitu muhimu bado hakijafanyika. Unahitaji nidhamu
binafsi ili kuweza kusimamia hili vizuri. Na hiki ndio kitakuwezesha kufikia
mafanikio.
TAMKO LA LEO;Najua kufanya vizuri kitu ambacho hakikutakiwa kufanyika kabisa ni upotevu mkubwa wa muda na kujidhulumu mafanikio. Kuanzia sasa sitafanya kitu ambacho hakina umuhimu kama kuna kitu muhimu sijakifanya bado. Hii ndio siri ya mafanikio na nitaifanyia kazi kila siku.
Tukutane kwenye
ukurasa wa 159 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na
maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi
mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Pia washirikishe
wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia
watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kujifunza zaidi ili
kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo
maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment