Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Saturday, June 13, 2015

UKURASA WA 164; Vitu Ambavyo Ni Rahisi Kufanya.... Na Madhara Yake.


Vitu ambavyo ni rahisi kufanya ndio vitu ambavyo havina thamani kubwa kwako. N vitu ambavyo hutakiwi kuviamini au kuvitegemea maana havitakupeleka kule ambapo unataka kufika.
Unapokutana na changamoto yoyote kuna njia mbili za kufuata, kupambana na changamoto hiyo, kitu ambacho ni kigumu kufanya na kinaweza kukuletea changamoto zaidi. Au unaweza kuikimbia changamoto hiyo kitu ambacho ni rahisi kufanya.
Kitu ambacho ni kigumu kufanya, kupambana na changamoto hiyo sasa kina nafasi kubwa ya kukuletea mafanikio. Lakini kitu ambacho ni rahisi kufanya, kukimbia changamoto hiyo kwa kulalamika au kuikataa kama vile haipo au haikuhusu hakuwezi kukuletea mafanikio kabisa. Kitu cha uhakika unachokuwa nacho ni kwamba kitu rahisi kufanya kitakupeleka kwenye matatizo zaidi.
SOMA; BIASHARA LEO; Kutojali Kwako Kunavyokuletea Hasara Kwenye Biashara.
Kwenye maisha, kazi na hata biashara, kitu ambacho ni rahisi kufanya hakiwezi kukuletea mafanikio makubwa na mara nyingi kitakuingiza kwenye matatizo zaidi
Baadhi ya vitu ambavyo ni rahisi kufanya na unatakiwa kuviepuka;
1. Kuongea sana badala ya kutenda.
2. Kukosoa.
3. Kutumia ulevi ili kuondokana na tatizo.
4. Kulaumu wengine.
5. Umbeya, masengenyo na majungu.
6. Kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi.
7. Kulala sana.
8. Kusema NDIO kwa kila jambo.
9. Kusema uongo.
10. Kuiba au kudhulumu wengine.
Acha mara moja kufanya vitu hivi ambavyo unaona ni rahisi lakini ndio vinazidi kukurudisha nyuma.
TAMKO LA LEO;
Vitu ambavyo ni rahisi kufanya ndio vimekuwa vinanizuia mimi kusonga mbele na kufikia mafanikio. Vitu hivi vimekuwa vinaniweka mbali zaidi na mafanikio na wakati mwingine kuniingiza kwenye matatizo makubwa zaidi. Kuanzia sasa nitaacha kukimbilia kufanya vitu ambavyo ni rahisi na kukabiliana na vile vigumu kwa sababu najua ndio vitakavyoniletea mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 165 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment