Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, June 10, 2015

UKURASA WA 161; Hiki Ndio Kinachokuzuia Wewe Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako.



Hakuna wakati bora wa kuwa hai kama sasa. Huu ni wakati bora sana kwa mimi na wewe kuwa hai hapa duniani. Hii ni kwa sababu kuna uhuru mkubwa sana wa kuweza kufanya kile ambacho kila mmoja wetu anapenda kufanya.
Huhitaji tena kupewa ruhusa ndio uweze kufanya kile ambacho unataka kukifanya. Unahitaji kujiruhusu wewe mwenyewe na kuanza kufanyia kazi mawazo yako na hatimaye yakakufikisha kwenye mafanikio makubwa sana.
Lakini pamoja na uhuru huu mkubwa bado watu wengi wanashindwa kujipa ruhusa na kusubiri mtu aje kuwapa ruhusa. Hili ni kosa kubwa sana linalowazuia wengi kufikia uwezo mkubwa ambao upo ndani yao.
Kama hutajiruhusu wewe mwenyewe hakuna atakayekuruhusu. Hii ni kwa sababu hao unaosubiri wakuruhusu hawajui ni nini hasa kipo ndani yako. Hivyo kuwategemea waweze kukitoa ni sawa na kupoteza muda wako bure.
Jipe ruhusa ya kuishi maisha ambayo unayataka na kuyafurahia na sio kuishi kwa sababu ndivyo wengine wanataka uishi. Una muda mchache sana hapa duniani, miaka 100 ijayo hutakuwepo hapa tena, hivyo haijalishi watu wengine wanakufikiriaje, haitadumu kwa zaidi ya miaka 100.
Ni afadhali uishi yale maisha ambayo ni bora kwako na huenda ukaacha alama kwenye maisha ya wengine na hata baada ya miaka hii 100 ukaendelea kukumbukwa. Ila kama utakuwa mtu wa kufuata kundi, kufanya kile ambacho kila mtu anafanya au anategemea ufanye hakuna kikubwa utakachofanya na hakuna atakayekukumbuka miaka 100 ijayo.

TAMKO LA LEO;
Najua nisipojipa ruhusa mwenyewe hakuna atakayenipa ruhusa. Ni mimi mwenyewe ninayejijua vizuri na ni kitu gani ninataka na ninaweza kufanya vizuri. Sitasubiri mtu anipe ruhusa, sitafanya kwa sababu kila mtu anafanya na sitafanya kwa sababu watu wanataka nifanye. Nitafanya kwa sababu ndio kitu hasa ninachotaka kufanya na ndio kitu ninachofurahia kufanya kwenye maisha yangu.

Tukutane kwenye ukurasa wa 162 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment