Unapokuwa unahitaji kufanya maamuzi ambayo huenda ni magumu kwenye kazi yako, biashara yako au hata maisha yako kwa ujumla, huwa unahitaji kupata ushauri. Unaweza kupewa ushauri mzuri sana kutoka kwa watu mbalimbali ambao unaweza kuwa unawaamini sana.
Pamoja na ushauri huu muhimu bado wewe mwenyewe ndio utahitaji kufanya maamuzi ya mwisho. Wewe ndio utakayekaa chini na kufanya maamuzi ambayo utakuwa tayari kuishi nayo.
Hivyo ni muhimu sana wewe uwe na uwezo wa kufanya maamuzi. Huwezi kutegemea tu watu watakavyokushauri, kwa sababu watu mbalimbali watakuwa na ushauri tofauti. Kama hutakuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi ambayo utakuwa tayari kuishi nayo, utaishia kufanya maamuzi ambayo yatakupoteza.
SOMA; Mambo Kumi(10) Unayotakiwa Kubadili Leo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.
Nakumbuka siku sio nyingi rafiki yangu mmoja aliniomba ushauri kuhusiana na maamuzi ya kibiashara aliyokuwa anataka kufanya. Nilimpa ushauri wangu na mambo muhimu anayohitaji kuzingatia. Baadae alinipigia kuniambia kwamba ameamua kufanya tofauti na nilivyomshauri. Nilistuka kidogo kwa sababu alichokuwa anakwenda kufanya ni kosa kubwa sana ambalo mimi binafsi nimewahi kufanya na likanigharimu na nimekuwa naona wengi wakifanya kosa hilo na linawagharimu sana. Nilijaribu kumwelewesha, labda kama hakuwa amenielewa vizuri, lakini alisisitiza kuendelea na kile alichopanga kufanya.
Nilijikumbusha kwamba yeye pekee ndio mwinye kufanya maamuzi ya mwisho na hivyo nilimwambia kila la kheri kama ndio maamuzi ambayo yuko tayari kuishi nayo. Siku chache baadae alinipigia na kuniambia hataendelea tena na mpango ule, hapa nilichanganyikiwa zaidi na sikutaka hata kujua zaidi.
Katika maisha yako jiandae kuweza kufanya mamauzi ambayo ni sahihi kwako na sio ya kusukumwa na mtu au kitu chochote.
TAMKO LA LEO;Tukutane kwenye ukurasa wa 181 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Najua ya kwamba nitapata ushauri kutoka kwa watu wengi. Najua ushauri huu utakuwa mzuri sana, lakini mwisho wa siku ni mimi pekee nitakayehitaji kufanya maamuzi ambayo ni sahihi kwangu na nitakuwa tayari kuishi nayo. Kila siku nitajijenga ili niweze kufanya maamuzi ambayo yatakuwa bora kwangu.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment