Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Monday, June 22, 2015

UKURASA WA 173; Maamuzi Uliyofanya Awali Na Maamuzi Mapya.

Mambo unayofanya sasa yanatokana na maamuzi uliyofanya awali. Na maamuzi haya uliyofanya awali yalitokana na uelewa uliokuwa nao kwa kipindi hiko unafanya maamuzi hayo.
Sasa swali linakuja kwako je sasa hivi bado una uelewa kama uliokuwa nao kipindi unafanya maamuzi? Kama jibu ni ndio basi endelea na kile unachofanya.
Kama jibu ni hapana, maana yake uelewa wako ni tofauti na ulivyokuwa zamani wakati unafanya maamuzi. Je kwa kuwa na uelewa wa tofauti sasa upo tayari kubadilika na kufanya maamuzi mapya ambayo yatakuwa bora zaidi?
Hili ni swali la msingi sana nakuuliza kwa sababu watu wengi wakishafanya maamuzi na kuona mambo yanakwenda vizuri wanajisahau, wanaendelea kufanya kile walichozoea kufanya mpaka wanapojikuta kwenye wakati ambao wanachofanya hakifai tena.
Mtu anaingia kwenye kazi lakini anaendelea kufanya kazi yake kwa mbinui zile zile alizokuwa anatumia awali. Wanakuja vijana wenye mawazo mapya na wanaweka mbinu mpya na mtu huyu anaanza kuchukia na kuona nafasi yake ipo hatarini.
Mtu anaingia kwenye biashara lakini miaka nenda miaka rudi anafanya kwa mbinu zile zile, wakija watu wapya na mbinu mpya wanamwondoa kwenye biashara ile anabaki kulia kwamba kafanyiwa mchezo mchafu.
Kadiri uelewa wako unavyoongezeka, boresha maamuzi yako na fanya mabadiliko yanayostahili. Dunia inabadilika, ni lazima na wewe ubadilike. Nafikiri umeona hapo nimekuambia NI LAZIMA ubadilike, sio unaombwa, ndivyo dunia inavyokutaka, la sivyo unaachwa nyuma, unapotezwa.
Kama mpaka sasa hujasoma kitabu, JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA unasubiri nini? Bonyeza hayo maandishi kujipatia kitabu hiki kitakachokuandaa vizuri na mabadiliko.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba maamuzi niliyofanya awali yalitokana na uelewa wangu kwa kipindi kile. Najua kwamba mpaka sasa uelewa wangu umebadilika na hata dunia imebadilika pia. Nahitaji kufanya maamuzi mapya kulingana na mabadiliko ya sasa na uelewa nilio nao. Na kuanzia sasa mabadiliko kwangu yatakuwa ni mara kwa mara, sitafanya kitu chochote kwa mazoea.
Tukutane kwenye ukurasa wa 174 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment