Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, May 3, 2015

UKURASA WA 123; Kazi Kama Bidhaa…

Kazi au shughuli yoyote unayofanya ni sawa na bidhaa iliyopo sokoni, kama thamani yake kwa sasa haikuridhishi, ongeza uhitaji wake na thamani yake itakua.

Watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba kazi wanayofanya inawapa kipato kidogo. Au biashara wanayofanya haiwapatii faida ya kutosha. Watu hawa huishia kulalamika tu bila ya kuchukua hatua yoyote.

SOMA; Jambo Moja Muhimu La Kuzingatia Ili Uwe Tajiri.

Sasa wewe usiwe mmoja wa walalamikaji hawa. Kama kazi au biashara unayofanya sasa haikupatii kipato cha kutosha kuna sehemu ambayo hujaweza kuifikia bado. Unahitaji kuongeza uhitaji wa kazi au biashara hiyo. Angalia jinsi ambavyo unaweza kuiboresha zaidi na kuwafikia watu wengi zaidi.

Kwa kufanya hivi utaweza kuongeza thamani, kupata faida kubwa na kufikia mafanikio makubwa.

SOMA; Hivi Ndio Vitu Vinavyopelekea Ongezeko La Thamani Ya Hisa Kwa Mwekezaji.

TAMKO LA LEO;

Kazi/Biashara ninayofanya ni bidhaa, kama ninachopata kwa sasa hakiniridhishi, nahitaji kuongeza thamani yake. Naweza kuongeza thamani yake kwa kuboresha zaidi na kufikia watu wengi zaidi.

Tukutane kwenye ukurasa wa 124 kesho.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment