Mara nyingi watu wamekuwa wakijiuliza kama kile wanachofanya ndio sahihi kwao na kwa jamii nzima inayowazunguka. Na kama mtu hana kipimo kizuri cha kujua kama anachofanya ni sahihi au la, basi anaweza kufanya mambo ambayo yatakuwa na madhara kwake na kw amaisha ya wengine.
Leo nakushirikisha njia rahisi ya kujua kama jambo unalofanya ni sahihi kwako na kwa jamii nzima inayokuzunguka. Kwa kufanya zoezi hili dogo kwenye kila jambo unalofanya utapata nafasi ya kujichunguza na kujisahihisha.
SOMA; Kama Umeajiriwa Na Hujaanza Kufanya Hili Jua Kuwa Unapotea.
Katika kila jambo ambalo unafanya kwneye maisha yako, kazi yako, na hata biashara yako, jiulize swali hili muhimu; KAMA NENO LANGU LENGEKUWA NDIO SHERIA YA DUNIA, JE DUNIA INGEENDELEA KUWEPO? Kabla hujaanza kufanya jambo lolote au kuendele akufanya jambo unalofanya, jipe sekunde chache za kujiuliza na kujibu swali hilo.
Kama neno lako lingekuwa ndio sheria ya dunia, yaani kile unachosema ndio watu wanafuata, kile unachofanya ndio kila mtu duniani anafanya, je dunia itakuwa sehemu salama ya kuishi. Je dunia itaendelea kustawi na watu kuishi vizuri.
Katika kazi unayofanya, fikiria kama kila mtu angekuwa anafanya kazi kama unavyofanya wewe, je kampuni au taasisi unayofanyia kazi ingekuwepo mpaka sasa? Katika biashara unayofanya pia, kama kila mtu angefanya biashara kama unavyofanya wewe je ungeikuta biashara hiyo, je biashara hiyo inaweza kwenda kwa miaka 50 ijayo? Kama jibu ni hapana maana yake kuna kitu unahitaji kurekebisha na ukishakirekebisha utakuwa umerudi kwenye njia ya kukupeleka kwenye mafanikio.
SOMA; Ni Sawa Kama Hutapata Kile Unachotaka.
Huwezi kufikia mafanikio makubwa kama unafanya jambo lolote la kuwaumiza au kuwadhulumu wengine. Najua walioshindwa watakuambia matajiri wote ni wanyonyaji, lakini sio kweli. Hakuna utajiri wa kweli unaotokana na unyonyaji, labda tafsiri yako ya unyonyaji iwe ni yako peke yako, kitu ambacho hatuwezi kukipinga.
Kuwa mwema, fanya mema na dunia itakuwa sehemu nzuri sana kwako na kwa viumbe wengine kuishi.
Like page yangu Coach Makirita Amani uendelee kujifunza mengi ya kuboresha maisha yako, kazi yako na biashara yako.
TAMKO LA LEO;
Kama kile ninachosema ndio kila mtu anafanya duniani, je dunia ingekuwa kwenye hali gani? Kama kile ninachofanya ndio kila mtu anakifanya je kazi ninayofanya au biashara ninayofanya ingekuwa kwenye hali gani? Nitakuwa mwema na kutenda mema ili niweze kufikia mafanikio na kuwezesha wengine kufikia mafanikio pia.
Tukutane kwenye ukurasa wa 134 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment