Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, May 20, 2015

UKURASA WA 140; Usiwasamehe Wazazi Wako, Waelewe…

Kuna watu wengi sana ambao wanaamini maisha yao yalivurugwa na maamuzi ambayo wazazi wao waliyafanya siku za nyuma wakati wao bado ni wadogo. Watu hawa wamekua wakiishi na imani hii kwa muda mrefu na inazidi kuwazuia wao kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao.

Kabla hata sijaweka maelezo mengi hapa, naomba ni seme hili moja kwa moja na ulielewe. Kama unavyosoma hapa una miaka zaidi ya 20, ni marufuku kutumia sababu kwmaba umasikini wako au matatizo yako yamesababishwa na wazazi wako, ni marufuku, tumeelewana? Kama ndio basi tuendelee na nikuambie ni kwa nini huna haki ya kutumia sababu hiyo.

SOMA; Kanuni Sita(6) Muhimu Za Kushinda Tatizo Lolote Unalokutana Nalo.

Ni kweli kwamba huenda maamuzi ambayo wazazi wako walichukua siku za nyuma yaliathiri sana nafasi yako ya kufanya vizuri kwenye maisha. Ila sasa haupo tena chini ya wazazi wako, kwa nini unaendelea kuwalalamikia? Tumia nafasi hii uliyonayo sasa kufanya kile ambacho ungependa kufanya kwenye maisha yako, hakuna tena wa kukupangia, ni wewe mwenyewe.

Huhitaji kuwasamehe wazazi wako, hawajakukosea, japo wewe unaona kuna makosa wamefanya kwako. Unahitaji kuwaelewa wazazi wako kwa sababu wakati wanafanya mamauzi ambayo unaona sasa yalikuathiri, hawakufanya kwa makusudi ili yakuumize, walifanya kwa nia njema tu, wakijua maamuzi hayo yatakuwa bora kwako. Kwa bahati nzuri wazazi wako nao ni binadamu kama binadamu wengine na wanakosea katika maamuzi mengi wanayofanya, hivyo moja ya maeneo waliyokosea ni hilo unaloona wewe. Hivyo waelewe hawa ni binadamu ambao walikuwa wanakutakia maisha mema lakini wakakosea kwenye mchakato mzima wa kukuletea wewe maisha hayo bora.

Sasa umeshakuwa mtu mzima, badala ya kupoteza nguvu zako kulalamika kwa nini wazazi wako walifanya walichofanya, wekeza nguvu hizo kwenye kutengeneza maisha unayotaka kuwa nayo. Na kuandaa maisha mazuri kwa watoto wako pia, japo na wewe utakosea na kuna uwezekano wakaja kukulaumu.

SOMA; Tabia Saba Za Watu Wasiokuwa Na Mafanikio.

Huna haja ya kuwasamehe wazazi wako, hawajakukosea, unatakiw akuwaelewa kwa sababu kuna maeneo walikosea, kama wanavyokosea binadamu wengine.

TAMKO LA LEO;

Kuanzia sasa nawaelewa wazazi wangu kwamba nao ni binadamu na kuna baadhi ya maamuzi yao juu yangu walikosea. Lakini siwezi kuendelea kulalamika kwa haya waliyokosea, mimi sasa ni mtu mzima na nitaweka nguvu nyingi kutengeneza maisha ninayoyataka mimi. Sihitaji kuwasamehe wazazi wangu, nahitaji kuwaelewa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 141 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.

Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.

Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.

Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.

Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment