Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Wednesday, April 1, 2015

NENO LA LEO; Hiki Ndio Unachohitaji Ili Kugeuza Ndoto Yako Kuwa Uhalisia.

“To turn your dreams into reality, all your resources, efforts and concentration should be aligned in the same direction.” ― Roopleen

Kugeuza ndoto yako na kuwa uhalisia, rasilimali zote ulizo nazo, jitihada zote na umakini wako wote vinahitaji kuwa kwenye uelekeo mmoja.

Ni vigumu sana wewe kutimiza ndoto zako kama hutaweka kila ulichonacho kwenye maisha yako kwenye ndoto hiyo.

Kama utagawa rasilimali zako na nyingine kuzielekeza sehemu nyingine, unazidi kuongeza muda ambao unahitaji ili kukamilisha ndoto hiyo.

Kama ilivyo kwenye mapambano au vita, kila mpambanaji anatakiwa kuweka rasilimali zote kwenye eneo moja ambalo ni adui. Hivyo na wewe weka rasilimali zako zote kwenye eneo moja ambalo ni kufikia ndoto zako.

Nakutakia siku njema.

SOMA; Jinsi Ya Kujijengea Uwezo Wa Kujiamini - 2

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment