Licha ya kuwa na malengo na mipango bado maisha yako yanahitaji kuwa na dhumuni. Dhumuni hili ni kile ambacho unataka maisha yako yawakilishe hapa duniani. Hivi ni vile ambavyo unataka maisha yako yawe kuhusiana na kile unachofanya.
Dhumuni lako kwenye maisha ndio litakaloendelea kukumbukwa hata pale utakapokuwa umeondoka kwenye dunia hii. Kwa mfano kama lengo lako ni kuwa na magari mawili, nyumba na mashamba, utakapoondoka kwenye dunia hii hakuna mtu atakayeendelea kusema mnamkumbuka Makirita, yule alikuwa na magari mawili, nyumba na mashamba? Habari kama hizi hazitasikika.
SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Vijana Wanaotafuta Ajira. Soma Hapa Uone Fursa Unazoweza Kutumia.
Kitakachosikika ni kile ambacho maisha yako yamefanikisha kukamilisha kwa ajili ya wengine. Zile alama ambazo umeacha kwenye maisha ya wengine. Hii itabaki milele na milele hata baada ya kuw aumeondoka kwenye dunia hii.
Dhumini lako kwenye maisha linatokana na maono yako kwenye maisha na linawahusisha watu wengine. Ni nini utakachofanya kwa ajili ya wengine? Hiki ndio kitakachokusukuma kuweza kufikia maono yako na dhumuni lako kwenye maisha.
Katika kazi yoyote au biashara yoyote unayofanya, unaweza kuacha alama kwenye maisha yako, fanya hili liwe dhumuni lako na angalia unaweza kutumia njia gani kufikia hilo.
SOMA; KITABU; Jinsi Ya Kufaidika Na Mabadiliko Yanayotokea Kwenye Maisha.
“DHUMUNI LANGU KWENYE MAISHA NI KUWASAIDIA WATU KUISHI MAISHA BORA NA YENYE MAFANIKIO KUPITIA MAFUNDISHO YANGU NA MAANDIKO YANGU.” Makirita Amani
TAMKO LA LEO;
DHUMUNI LANGU KWENYE MAISHA NI _________________________________________________________________________________________________________________________ andika dhumuni lako hapo na uanze kulifanyia kazi kila siku kwenye maisha yako na kazi zako.
Tukutane kwenye ukurasa wa 110 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment