Katika jambo lolote la tofauti ambalo utajaribu kufanya, kuna watu wengi sana watakupa maoni yao. Wengi watakukatisha tamaa na kukuambia huwezi. Na wataenda mbali zaidi na kukupa mifano ya watu waliojaribu na wakashindwa.
Lakini kuna habari njema sana kwako. Na habari hizi ni kwamba hakuna atakayewakumbuka watu hawa. Baada ya muda watakuwa wamepita na hakuna sehemu yoyote ambapo watakuwa wameandikwa kama kumbukumbu.
SOMA; Hizi Ndizo Gharama Unazotakiwa Kuzilipia, Ili Uweze Kupata Kile Unachokihitaji Katika Maisha Yako.
Wakati Mwalimu Nyerere anapigania uhuru wa nchi kuna watu walikuwa wanamwambia asijisumbue, hawa wakoloni hawatakuachia. Lakini leo tunamjua Nyerere na hao wengine hatujawahi hata kuwasikia.
Wakati Thomas Edison anatengeneza taa ya umeme watu wengi walimwambia kwamba anachojaribu kufanya hakiwezekani. Lakini leo hii tunamjua Edison na hao wengine hatuna habari nao.
Henry Ford aliwaambia mainjinia wake watengeneze V8 engine, kitu ambacho hakikuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa uinjinia. Mainjinia wale walimwambia hiko ni kitu ambacho hakiwezekani. Aliwasisitiza wafanye hivyo. Leo hii tunaijua V8 na tunamjua Ford lakini wale mainjinia na wengine waliokuwa wanampinga hatuwajui.
SOMA; Haya Ndio Matumizi Mazuri Ya Mshahara Wako Ambayo Yatakuletea Furaha Na Mafanikio.
Ukweli ni kwamba jambo lolote unalotaka kufanya, watu watakupinga. Kama utawasikiliza na kuacha, wote mtasahaulika. Lakini kama utakataa kuwasikiliza na kuendelea kufanya, utaleta mabadiliko na utaendelea kukumbukwa hata utakapokuwa umekufa. Na wale waliokuwa wanakupinga, hakuna atakayekuwa na muda nao. Kwanza hakuna atakayejua kama hata walikuwepo.
Usitishwe na watu wanaokukatisha tamaa, sio watu watakaoingia kwenye vitabu vya historia, achana nao, endelea kupambana.
TAMKO LA LEO;
Watu wote wanaonikatisha tamaa ni watu wadogo sana kwangu na hawawezi kuingia kwenye kitabu chochote cha historia. Kama nikiwasikiliza na kukata tamaa nitakuiwa sawa na wao. Ila kama sitawasikiliza na kuendelea na malengo na mipango yangu, siku zijazo nitakuwa sehemu ya histiria wakati wao watakuwa wamesahaulika.
SOMA; Hii Ndio Njia Moja Muhimu Ya Kufikia Mafaniko Makubwa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 102 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment