Kama NINGEanza biashara kipindi kile nilipokuwa na kazi na nguvu bado, leo maisha yangu yangekuwa bora sana….
Kama NINGEchagua kuishi maisha ninayotaka kuishi mimi na sio maisha ya kuiga, leo hii nisingejikuta kwenye matatizo makubwa….
Kama NINGEpata muda wa kutosha wa kukaa na wale ninaowapenda, maisha yangu yangekuwa na furaha zaidi….
Kama NINGEchagua kutokukata tamaa, kuweka juhudi na maarifa katika kile nilichochagua kufanya, leo hii ningekuwa mbali sana….
Haya ni baadhi ya mambo ambayo watu wengi huwa wanajutia hasa pale ambapo maisha yao yanakuwa yameshafika ukingoni.
SOMA; KURASA YA 01; Maisha Unayoishi Ni Yako.
Kama unasoma hapa, kuna uwezekano mkubwa bado hujafikia hatua hii ya kuwa na majuto, lakini huenda umejisahau, na miaka 10, 20, au 30 ijayo, utakaa chini na kusema mija ya kauli hizo hapo juu.
Hakuna kitu kinaumiza kwenye maisha kama majuto. Hakuna kitu kinaumiza kama kujua wkamba ulikuwa na nafasi ya kufanya maisha yako yawe bora ila hukuichukua.
Ndio maana leo nakuambia kwamba, acha kutengeneza mazingira ambayo yatakufanya ujute sana baadae.
Chagua kufanya kazi au biashara unayoipenda, katika wakati huu ambao bado una nguvu za kuwez akupambana. Jali afya yako na ilinde sana maana hii ndio kila kitu kwako. Tengeneza mahusiano yako vizuri na watu wa karibu kwako, maana hawa ndio wanaokufanya uwe na maisha ya furaha.
SOMA; Ni Lipi Dhumuni Lako Kwenye Maisha? Langu Ni Hili Hapa.
Usijiweke kwenye mazingira yatakayokufanya wewe uwe na majuto baadae. Utaona maisha yako hayakuwahi kuwa na maana kabisa.
TAMKO LA LEO;
Najua mambo mengi ninayoyapuuza kwa sasa yatakuja kuwa sehemu ya majuto yangu hapo baadae. Kuanzia sas anayabadili maisha yangu, naishi maisha ambayo yana maana kwangu, nitafanya kile ninachopenda, nitajali afya yangu na kujenga mahusiano mazuri na wale ambao ni wa karibu kwangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 112 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment