Kila mmoja wetu ana uwezo mkubwa wa kuibadili dunia. Kila mmoja ana eneo lake ambalo kama akiweza kulitumia vizuri itakuwa faida kwake mwenyewe na kwa wengi wanaomzunguka.
Je wewe umeshapanga kuibadili dunia? Au unataka kuibadili dunia?
Kama ndio karibu, na kama hujui uanzie wapi basi leo unapata pa kuanzia.
SOMA; Sababu 10 Kwa Nini Hutafikia Malengo Yako 2015.
Amua kwamba unakwenda kuibadili dunia kupitia kile ambacho unafanya au unataka kufanya. Kila kitu kinachofanyika na binadamu kina uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kwenye dunia. Iwe ni biashara, kazi au hata huduma yoyote ambayo mtu anaweza kuitoa.
Ukishaamua ni jinsi gani unakwenda kuibadili dunia, wekeza nguvu na jitihada zako zote kwenye kile unachofanya ili kuibadili dunia. Utakapofanya hivi, vitu viwili vinaweza kutokea.
1. Unaweza kufanikiwa kwa kila hatua na hapa tumia mafabikio haya kama motisha wa wewe kuendelea zaidi.
2. Unaweza kukutana na changamoto na kushindwa kwenye baadhi ya hatua, na hapa tumia changamoto hizi kujifunza zaidi ila usiache au kukata tamaa.
SOMA; Huu Ni Uwekezaji Wa Uhakika Ambao Hautakuangusha.
Lengo lako la mwisho ni kuibadili dunia, hayo mengine yote siyo ya msingi, usikubali yakupotezee muda.
TAMKO LA LEO;
Nimeamua sasa nakwenda kuibadili dunia kupitia_______________(sema kile unachofanya au utakachofanya). Nitaweka juhudi na maarifa katika lengo hili na mafanikio nitakayopata nitayatumia kujihamasisha. Pia changamoto nitakazokutana nazo nitazitumia kama sehemu ya kujifunza. Nitakomaa na lengo langu hili, mengine yote yanaweza kusubiri.
Tukutane kwenye ukurasa wa 105 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment