Fursa Fursa Fursa…..
Katika wakati wowote ule kwenye maisha yako na katika jambo lolote unalofanya, kuna fursa nyingi sana ambazo zimekuzunguka. Na kama ukiwa macho ndio fursa zinazidi kuwa nyingi.
Kwa kuwa wewe ni mtu ambaye unataka kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa inabidi uzichangamkie fursa hizi, si ndio?
Kama utaichangamkia kila fursa, unajiandaa kushindwa kufikia mafanikio. Haijalishi una uwezo mkubw akiasi gani, haijalishi una kiu kiasi gani ya kufikia mafanikio, kujiingiza kwenye fursa nyingi kutakuwa kikwazo kikubwa kwako kufanikiwa.
SOMA; Haya Ndiyo Mambo Yanakukwamisha Na Kukufanya Ushindwe Kufikia Malengo Yako Uliyojiwekea.
Kama utaikimbilia kila fursa ambayo unaiona, utaishia kukimbiza ndoto za watu wengine huku ukisahau kabisa ndoto zako.
Chagua aina ya fursa ambazo unaweza kuzifuatilia na nyingine zote achana nazo. Mtu anayekimbiza sungura mmoja ana uwezekano mkubwa wa kumkamata. Mtu anayekimbiza sungura wawili hawezi kumkamata hata mmoja.
Hakikisha fursa unazofuatilia zinakuwa sungura mmoja ili uweze kufikia ndoto zako.
TAMKO LA LEO;
Najua kuna fursa nyingi sana zinazonizunguka. Pia najua siwezi kuzikimbilia fursa zote, na kw akujaribu hivyo itanizuia mimi kuweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yangu. Nitachagua aina ya fursa za kufuatilia na nyingine nitaachana nazo.
SOMA; Dalili Za Kuanguka, Zijue Na Jinsi Ya Kuepuka.
Tukutane kwenye ukurasa wa 114 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment