Palikuwepo na tawala kubwa sana duniani na zenye nguvu ila zote zilianguka pale ambapo zilikuwa kwenye mafanikio makubwa. Mifano ya tawala hizo ni Roma, Misri, Babeli na nyingine nyingi.
Palikuwa na watu ambao walikuwa na mafanikio makubwa sana kwenye kile wanachofanya. Kuna ambao walikuwa wachezaji maarufu, wengine waimbaji, wengine wafanyabiashara ila wengi walianguka wakati ambao ndio walikuwa na mafanikio makubwa.
SOMA; Siri Kubwa Unayotakiwa Kujua Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara.
Haya yalitokea na hata sasa yanaendelea kutokea na usipokuwa makini yatatokea na kwako pia.
Unaweza kukazana sana sasa hivi kufikia mafanikio makubwa ila pale utakapoyapata ukaanguka na kupotea kabisa.
Ni muhimu wewe kujua dalili za kuanguka na dalili moja kubwa ni kuridhika. Pale unapoanza kujiona umeridhika, unapozoea mafanikio, unapoanza kuona wewe ndio kila kitu, hapo ndio unafanya makosa makubwa sana na utaanguka.
SOMA; Sifa Moja Muhimu Ambayo Kila Kiongozi Mkubwa Anayo.
Hata uwe umefikia mafanikio makubwa kiasi gani, usiache kufanya yale yaliyokufikisha kwenye mafanikio hayo. Endelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, endelea kuwa muaminifu, endelea kujifunza, endelea kushirikiana na watu na mafanikio yako yatakuwa ni ya kudumu.
TAMKO LA LEO;
Najua dalili za kuanguka ni pale nitakapoanza kujiona mimi ndio kila kitu, nitakapoanza kuacha kufanya yale ambayo yamenifikisha kwenye mafanikio. Hapo nitaanza kuporomoka kwa kasi. Ili kuepuka hili nitaendelea kufanya yale ninayofanya bila kuchoka au kujiona nimefika juu sana.
SOMA; Dalili Kumi Kwamba Tayari Wewe Ni Kiongozi.
Tukutane kwenye ukurasa wa 67 kesho.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment